Wasanii mbalimbali wakifuatilia mjadala kwenye ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) |
Msanii akipiga tarumbeta |
HEBU fikiria, unaamka asubuhi na mapema,
unajiandaa na kubeba begi lako kisha unaelekea kituo cha basi, unalikuta gari na
kupanda, lakini hujui unaelekea wapi!
Au mpo katika kituo cha mabasi, mara basi linakuja,
kila mmoja analikimbilia na kupanda, tena mnafikia hatua ya kugombea siti, na
safari inapoanza ndipo mnagundua kuwa gari haliendi kule mnakokwenda. Mnataharuki na kuanza kumpigia kelele dereva
kumtaka asimamishe gari!
Dereva anawashangaa na analiegesha gari pembeni,
kisha anawauliza kwani ninyi mnaelekea wapi? Hapo ndipo mnapojigundua kuwa kila
mmoja anaelekea sehemu tofauti kabisa na linakokwenda gari!