Naibu Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo,
Juma Nkamia
Alhamisi wiki hii, Wizara ya
habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ilisoma bajeti yake ya mwaka 2014/15 na
kuweka vipaumbele vyake. Lakini pamoja na kuigusa sekta ya filamu bado imekuwa
haipewi kipaumbele japo imeonekana kuchangia kwa kiasi kikubwa katika ajira na
pato la Taifa.
Tanzania ni moja ya nchi
chache zenye maeneo mazuri ya kuvutia yanayofaa kabisa kwa kutengenezea filamu,
ni nchi yenye wasanii wengi wazuri wenye vipaji lakini waliokosa muongozo.
Tasnia ya filamu na muziki nchini ni sekta tajiri sana lakini zisizopewa
kipaumbele.