Dec 28, 2016

Wasanii mmejipangaje kwa mwaka 2017?

· Ni wakati sasa mfikirie kuwa na dira

Wafanyuakazi wa Mamlaka ya Mapato (TRA) walipotembelea wauzaji wa filamu za Tanzania kuhakiki kazi zenye stempu za TRA

Mmoja wa wasanii wa filamu Tanzania, Vicent Kigosi, maarufu kama Ray

KWA Tanzania hakuna msanii yeyote anayeweza kusimama na kujisifu kwamba anakula halali kulingana na wingi wa jasho lake. Kila mmoja anatambua kuwa kuna mfumo kandamizi unaonyonya jasho la wasanii. Na ili kuendelea kuwanyonya, sasa wameaminishwa (na wale waliolishika soko) kuwa soko la kazi zao limekufa.

Wameaminishwa hivyo kwa kuwa soko la kazi zao linadhibitiwa na wafanyabiashara wachache, wasiozingatia taaluma na wasioongozwa na weledi. Ki ukweli kwa sasa soko halieleweki kabisa! Hali hii imesababisha watu kushindwa kutofautisha iwapo wanachokiona ni filamu, maigizo au mkanda wa harusi wenye “taito” za majina ya wasanii na wafanyabiashara wenye asili ya Kiasia!

Sep 28, 2016

MAFUNZO KWA WAANDISHI: Pongezi kwa Bodi ya Filamu Tanzania

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fissoo, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Waandishi wa Filamu kwa baadhi ya waandishi hao Jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

MWANDISHI mzuri wa filamu ni lazima awe na kipaji na uwezo mzuri wa kuandika. Kipaji mtu huzaliwa nacho au hukipata (adapt) katika umri mdogo kutokana na mazingira anayokulia. Uandishi mzuri wa filamu huanzia katika kuwa na uwezo wa kuumba maneno ambayo yatakuwa rahisi kueleweka pindi mtu akiyasikia.

Wakati unaandika ni muhimu sana kuzama ndani ya akili za walengwa wako ujue wanataka nini.

Sep 14, 2016

Tutumie filamu na nyimbo kuhamasisha uzalendo

Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Filamu, Bi Joyce Fisso
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo . Nape Nnauye akipata maelezo juu ya utamaduni wa kucheza bao kwenye kituo cha Utamaduni wa kisukuma Bujora
TUNAELEKEA kutimiza miaka 55 tangu tuwe huru, lakini bado jamii ya Kitanzania imeendelea kupoteza maadili, mila na tamaduni zake kila kukicha. Baada ya uhuru wa Tanganyika mwaka 1961, Wizara ya Utamaduni wa Taifa na Vijana iliundwa mwaka 1962, rais wa wakati huo, Mwalimu Julius Nyerere, ambaye alitamka wazi kuwa Utamaduni ndiyo kiini na roho ya Taifa, na nchi inayokosa utamaduni wake ni sawa na mkusanyiko wa watu usiokuwa na roho na hivyo kukosa sifa ya kuitwa taifa kamili.

Aug 31, 2016

Bongo Movies: Bado tuna tatizo kubwa katika uandishi wa filamu

Mwandishi wa makala haya, Bishop Hiluka, katika moja ya kazi za uandishi wa filamu

FILAMU ni chombo muhimu sana cha mawasiliano katika jamii na ustawi wa nchi yoyote, huchangia kupatikana kwa ajira kwa vijana, huchangia ukuaji wa uchumi wa nchi, husaidia kuwaambia watu wengine kuhusu hadithi za jamii husika, huchangia maendeleo ya nchi na kadhalika.

Utengenezaji wa filamu si suala la mzaha, si jambo la mtu ambaye jana usiku alilala akiwa hana kazi ya kufanya na leo asubuhi kaamka akiwa na wazo la kutengeneza filamu, bila kuwa na ujuzi, nyenzo wala mtaji wa kutosha. Utengenezaji filamu ni jambo linalohitaji gharama, ni jambo la hatari (venture) linalohitaji muda mwingi na mtengenezaji wa filamu hatakiwi kuwa mvivu wa kufikiri au kupoteza muda akipiga soga na rafiki zake au kufanya mizaha.

Jul 29, 2016

Waziri Nape Nnauye; Angalia pia upande wa pili wa shilingi

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, akiwa katika Operesheni ya kuwasaka waharamia wanaodurufu kazi za wasanii
SERIKALI ya Awamu ya Tano imeanza kuonesha juhudi katika kuisaidia sekta ya sanaa nchini baada ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, kuingia mtaani na kukamata DVDs zisizo na stika ya TRA zinazoingia nchini kinyume na sheria pamoja na zile zinazokwepa kulipa kodi ili kuinua uchumi wa nchi na wasanii.

Waziri Nape Nnauye ameahidi kuwa zoezi hilo litakuwa endelevu nchi nzima akisisitiza kuwa hatua hii ni ya mwanzo kwa kuwaonesha kuwa agizo la Rais John Pombe Magufuli, la kulipa kodi na kununua bidhaa halisi kwa kutoa risiti linasimamiwa ipasavyo.

Jun 22, 2016

Kipindi cha XYZ cha Kenya kumilikiwa na Trace TV


Kipindi hiki kinachohitajika sana kimekuwa kikiimarika katika bara Afrika. Mapema mwaka huu kulikuwa na uzinduzi wa Netflix katika soko la Afrika, hatua iliyofurahisha wateja wengi. Hatua hii inajiri wakati ambapo Showmax cha Afrika Kusini kinatarajiwa kuingia katika soko la Kenya. Mipango mengine ni ile ya ushirikiano wa kati ya Airtel na Ericsson kuzindua huduma kwa jina NUVU.

Jun 8, 2016

Mgogoro TAFF ni vita vya panzi, furaha kwa kunguru

Kutoka kushoto; Katibu Mtendaji wa BASATA Godfrey Mungereza, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Joyce Fisoo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel, na Rais wa TAFF Simon Mwakifwamba. Hii ilikuwa ni siku ya uzinduzi wa Tuzo za TAFA

NIKIWA sijui hili wala lile hivi karibuni nilijikuta natumiwa ujumbe wa WhatsApp kwenye simu yangu kutoka kwa mdau mmoja wa filamu. Ujumbe ambao nilipoutazama kwa makini nikagundua kuwa haukuwa umeandikwa na mdau aliyenitumia bali ama alitumiwa au aliukopi kutoka kwa mdau mwingine.

Ujumbe huu uliandikwa hivi: “Habari? Mungu hulipa hapa hapa, tulimpakazia Bishop kila aina ya hila kulinda mambo yetu lakini tukajiona washindi bila kujua dhambi kubwa tuitendayo itatuhukumu tulipo. Kwa tatizo hili la Tanzanite film festival, Katibu tena atang’oka? Nasubiri muujiza. Hongera sana ndugu yangu Bishop, dhuluma uliyofanyiwa inawahukumu.”

Mar 30, 2016

Tunamisi burudani za majumba ya sinema

Watu wakiangalia sinema
LEO nimekumbuka mbali sana, hasa baada ya kupita sehemu na kuwasikia wanafunzi wa shule ya msingi (wenye miaka isiyozidi kumi), ambao wapenzi wa sinema, wakisimuliana na kubishana kuhusu kina Ray, Kanumba, Gabo nk. Ndipo nikakumbuka nilipokuwa katika umri huo tulikuwa pia tukisimuliana na kubishana kuhusu kina Amitabh Bachchan, Mithun Chakrabot, Amjad Khan, DharmendraSanjeev Kumar, Charlie Chaplin, nk.

Wakati huo hatukuwa na vituo vya televisheni kama leo. Vituo vya televisheni Tanzania Bara televisheni vimeanza mwanzoni mwa miaka ya 1990. Hadi 1996 kulikuwa na vituo vitatu tu vya CTN, DTV na ITV. Hata hivyo, televisheni imekuwapo Zanzibar tangu mwaka 1973.

Mar 2, 2016

LEONARDO DICAPRIO: Avumilia miaka 6 kushinda Tuzo ya Oscar


TUZO za Oscar (The Academy Awards), huwakilishwa kila mwaka na kampuni ya Academy of Motion Picture Arts and Sciences (Kifupi: AMPAS) kwa lengo la kutambulisha taaluma ya tasnia ya filamu, wakiwemo waongozaji, waigizaji, na watunzi wa filamu. Rasmi huwa sherehe za utoaji wa tuzo mbalimbali. Pia inasemekana kuwa ni miongoni mwa sherehe zinazotazamwa sana duniani mara tu sherehe hizo zinapoanza.

Katika Tuzo za mwaka huu mwigizaji nyota wa Hollywood, Leonardo DiCaprio, hatimaye amejishindia tuzo yake ya kwanza ya Oscar kwa uigizaji wake katika filamu ya ‘The Revenant’, baada ya kushindania tuzo hizo mara sita. Amekuwa mwigizaji bora kwenye Tuzo za 88 za Oscar.

Nani kaiua Sekta ya Filamu ya Tanzania?

Afisa kutoka Bodi ya Filamu Tanzania, Wilhad Tairo, akifafanua jambo kwa mfanyabiashara wa duka la Filamu wakati wa Operesheni ya kukagua Bidhaa zisizo na stika za TRA
Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu Tanzania, Sylvester Sengerema

HALI ya Sekta ya Filamu ya Tanzania kwa sasa ni mbaya sana. Ninathubutu kusema kwamba sekta hii ipo ukingoni mwa kifo, kilichobaki ni ung’ang’anizi tu. Ikumbukwe kuwa mzunguko wa maisha hufuata hatua nne: kuzaliwa, kukua, kukomaa na kuzeeka kabla ya kifo, ambapo kama hakuna matatizo, tunategemea mwanadamu kufa baada ya hatua hizo.

Feb 26, 2016

Tony Burton, mcheza sinema za Rocky afariki

Tony Burton (kushoto) akiwa na Sylvester Stallone (Rambo)

Tony Burton aliyeshiriki katika filamu sita za Rocky dhidi ya Sylvester Stallone, amefariki akiwa na umri wa miaka 78. Kiini cha kifo chake bado hakijulikani, lakini dada'ake, Loretta Kelly, amesema kuwa amekuwa akienda hospitalini katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Ameongozea kuwa hajapata utambuzi wa ugonjwa wake katika wakati huo na kwamba hali yake ya afya ilikuwa imezorota hali ya kutoweza kuiona filamu ya Creed.

Uigizaji wake ulimsaidia Creed ambaye ni mpinzani wa Rocky Balboa katika filamu mbili za kwanza za masumbwi kabla ya kuwa mkufunzi wa Balboa.