TUZO za Oscar (The
Academy Awards), huwakilishwa
kila mwaka na kampuni ya Academy of Motion Picture Arts and Sciences (Kifupi:
AMPAS) kwa lengo la kutambulisha taaluma ya tasnia ya filamu, wakiwemo
waongozaji, waigizaji, na watunzi wa filamu. Rasmi huwa sherehe za utoaji wa tuzo mbalimbali. Pia
inasemekana kuwa ni miongoni mwa sherehe zinazotazamwa sana duniani mara tu
sherehe hizo zinapoanza.
Katika Tuzo za
mwaka huu mwigizaji nyota wa Hollywood, Leonardo DiCaprio, hatimaye
amejishindia tuzo yake ya kwanza ya Oscar kwa uigizaji wake katika filamu ya ‘The
Revenant’, baada ya kushindania tuzo hizo mara sita. Amekuwa mwigizaji
bora kwenye Tuzo za 88 za Oscar.
Leonardo DiCaprio ni muigizaji wa
Marekani ambaye alianza fani ya uigizaji akiwa mdogo kwenye televisheni. Mwaka 1989 alionekana
kwenye kipindi cha ‘Lassie New’
na 1990 kwenye ‘Santa Barbara’
na pia mwaka huohuo aliigiza katika michezo ya vichekesho ya ‘Parenthood’ na ‘Growing Pains’
mwaka 1991, kabla ya kufanya filamu yake ya kwanza mwaka 1991, ya ‘Critters 3’.
Miaka miwili baadaye 1993,
alicheza katika ‘This Boy’s Life’. Baadaye mwaka huohuo akacheza kama muigizaji msaidizi katika
filamu ya ‘What’s Eating Gilbert Grape’, ambayo ilimwezesha kuteuliwa katika Tuzo ya Academy
kama Muigizaji Bora Msaidizi. Mwaka 1995, DiCaprio alicheza kama mwandishi wa
Marekani, Jim Carroll, katika filamu ya ‘The Basket Diaries’ na Mshairi
wa Kifaransa, Arthur Rimbaud katika ‘Total Eclipse’.
Mwaka uliofuata 1996 alicheza kama Romeo Montague
katika filamu ya Romeo & Juliet
ya Baz
Luhrmann. Mwaka 1997 DiCaprio aliigiza pamoja na Kate Winslet katika filamu ya James
Cameron ya Titanic. Filamu
iliyokuwa na mapato ya juu sana duniani kote kwa mauzo ya teketi, na kumpa
umaarufu mkubwa duniani.
Titanic ni filamu
ya kusikitisha na ya mapenzi inayohusu kuzama kwa meli ya Titanic. Filamu hii
iliongozwa, ikaandikwa, ikatayarishwa na kuhaririwa na James Cameron mnamo
1997. Wahusika wake ni Leonardo DiCaprio kama Jack Dawson na Kate Winslet kama
Rose DeWitt Bukater. Wawili hawa wenye maisha tofauti walipendana walipokutana
kwenye meli hii ambayo haikuwa na mwisho mwema.
Filamu hii ambayo ilikuwa itolewe mnamo 2 Julai 1997
lakini tarehe ikapelekwa mbele hadi 19 Desemba 1997. Ilipata mafanikio makubwa,
kwa kushinda tuzo kumi na moja za Academy Awards. Pia alicheza sinema ya ‘Man in the Iron Mask’ mwaka 1998.
Kwa
uigizaji wake, alipata Tuzo ya Muigizaji Bora wa Kiume wa MTV na uteuzi wake wa
kwanza kwa Tuzo ya Golden Globe kama Muigizaji Bora - Motion Picture
Drama.
Mwaka
2002, DiCaprio alicheza kama tapeli (con-artist) Frank Abagnale Jr. mpinzani wa Tom Hanks katika sinema iliyoongozwa na Steven
Spielberg ya kihalifu inayoitwa ‘Catch Me If You Can’ na pia kuwa nyota katika sinema
iliyoongozwa na Martin Scorsese ya ‘Gang of New York’.
Alianzisha
kampuni yake mwenyewe ya uzalishaji, Appian Way, mwaka 2004. Filamu mbili zilizofuata
aliigiza kama nyota ambapo zote mbili ziliongozwa na Scorsese: ‘Howard Hughes biopic The
Aviator’ (2004)
na ya kihalifu ‘The Departed’ (2006). Kwa uigizaji wake, DiCaprio
alishinda tuzo ya Golden Globe kwa Muigizaji Bora – ‘Motion Picture Drama’ na kufanikiwa
kuteuliwa kwa mara ya kwanza kwa ajili ya Tuzo ya Academy kama Muigizaji
Bora. Na sinema ya kutisha ya vita vya
kisiasa ya Blood Diamond mwaka 2006.
DiCaprio
alitoa filamu ya makala (documentary) ya mazingira ‘The 11th Hour’ na ya vichekesho ya ‘Gardener of Eden’ mwaka 2007. Mwaka uliofuata, aliungana
tena na Kate Winslet katika sinema ya ‘Revolutionary
Road’ iliyoongozwa na Sam Mendes, na akaonekana katika sinema ya ‘Body
of Lies’ iliyoongozwa na Ridley Scott. DiCaprio aliungana tena na Scorsese
mwaka 2010 katika sinema ya kutisha ya kisaikolojia ya Shutter Island na pia akacheza kama nyota katika sinema iliyoongozwa na Christopher
Nolan ya ‘Inception’.
Mwaka
2011, alimuigiza J. Edgar Hoover, mkurugenzi wa kwanza wa FBI. Mwaka uliofuata, alicheza
muigizaji msaidizi katika sinema iliyoongozwa na Quentin Tarantino, ‘Django Unchained’. DiCaprio aliigiza katika filamu
mbili zilizotokana na riwaya mwaka 2013; kwanza alionekana kama Jay Gatsby katika sinema
iliyoongozwa na Luhrmann iliyotokana na riwaya ya F. Scott Fitzgerald ya ‘Great Gatsby’, na baadaye kama Jordan Belfort katika sinema ya ‘Wolf
ya Wall Street’, iliyotokana na riwaya ya
Belfort yenye jina kama hilo. Mwisho ilimwezesha kuteuliwa kwa mara
ya tatu kuwania Tuzo za Academy kama Muigizaji Bora na Tuzo za Golden
Globe kama Muigizaji Bora – ‘Motion Picture Musical or Comedy’
Jina lake kamili ni Leonardo Wilhelm DiCaprio, amezaliwa mnamo 11 Novemba 1974 katika
eneo la Hollywood,
California, ni mtoto pekee wa Irmelin (nee Indenbirken), mzaliwa wa Ujerumani
ambaye ni katibu wa sheria, na George DiCaprio, msanii wa uchoraji (comic artist)
na mtayarishaji na msambazaji wa vitabu vya Comic (hadithi za michoro). Baba
yake DiCaprio ana asili ya kutoka ukoo wa Kitaliano (kutoka eneo la Naples) na Kijerumani (kutoka Bavaria).
Wazazi
wa DiCaprio walikutana wakati wakisoma chuo na hatimaye wakahamia Los Angeles.
Yeye aliitwa jina lake Leonardo kwa sababu mama yake alipokuwa mjamzito alikuwa
akiuangalia sana mchoro wa Leonardo da Vinci katika
makumbusho nchini Italia wakati DiCaprio aliporukaruka tumboni. Wazazi wake walitalikiana
wakati DiCaprio alipokuwa na mwaka mmoja, na baadaye aliishi zaidi na mama yake. Waliishi katika vitongoji vya Los
Angeles, kama vile Echo Park, na 1874 Hillhurst Avenue, wilaya ya Los Feliz (eneo ambalo baadaye lilibadilika
kuwa maktaba za umma), wakati huo mama yake akifanya kazi kadhaa kwa ajili ya
kujikimu yeye na mwanaye.
DiCaprio
alisoma katika Shule ya Seeds Elementary (kwa sasa UCLA Lab School) na masomo ya sekondari
katika shule ya John
Marshall high School, mita chache tu, baada ya masomo Los Angeles Centre for
Enriched Studies kwa miaka minne. Hata hivyo, aliacha shule akiwa shule ya
sekondari katika mwaka wake wa tatu, hatimaye akapata stashahada. DiCaprio aliishi
sehemu ya maisha yake ya utoto nchini Ujerumani kwa bibi na babu wa upande wa
mama yake, Wilhelm na Helene.
DiCaprio
anaongea kidogo Kijerumani na Kitaliano.
No comments:
Post a Comment