Aug 29, 2011

NAOMI: Filamu ya mwisho ya marehemu Tabia

Marehemu Dalillah Peter Kisinda (Tabia)

 Kava la filamu ya Naomi (part 2)

TASNIA ya filamu nchini mwetu imezidi kukua na kuendelea kuua soko la filamu kutoka Nigeria ambazo mwanzoni mwa miaka ya 2000 zilikuwa zimeliteka soko la nchi yetu. Tofauti na ilivyokuwa miaka michache iliyopita, kwa sasa takriban, filamu mbili mpya za Kitanzania hutoka kila wiki na hali inaonesha kwamba idadi hiyo itazidi kupanda miaka michache ijayo, hasa kama watengeneza filamu wa Tanzania wataboresha zaidi kazi zao.

Moja ya filamu inayosubiriwa kwa hamu ni ya Naomi, iliyotayarishwa na mmoja wa Watunzi mahiri wa hadithi nchini na mtengeneza filamu, Hamisi Kibari.

Aug 25, 2011

Kwa nini uuze haki yako?

Mtendaji Mkuu wa Cosota, Yustus Mkinga, akifafanua jambo mbele ya wadau wa sanaa wakiwemo waigizaji wa filamu hapa nchini, kuhusiana na suala la hakimiliki za wasanii

NASHUKURU sana kwa makala yako ambayo imenielimisha mambo mengi kuhusu tasnia ya filamu ingawa nina wasiwasi unaposema kuwa Serikali ya Tanzania haielewi ukubwa wa biashara hii, kama haielewi mbona Rais Jakaya Kikwete aliwahi kutamka bungeni kuwa tasnia ya filamu Tanzania inakua na akaahidi kuwasaidia wasanii...?”

Huu ni ujumbe nilioupata kutoka kwa msomaji mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Jonas Komba, mkazi wa Iringa aliyeonekana kunishangaa nilipoandika kuwa serikali haijui ukubwa wa biashara ya filamu.

Aug 18, 2011

Hatuibiwi... Haki ya Mungu tunaibiwa!

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, 
Dk. Emmanuel Nchimbi
ASUBUHI moja naamka na kwenda panapouzwa magazeti ili nipate kujua kinachoendelea hapa nchini na duniani kupitia magazeti, kama kawaida nasoma kwanza vichwa vya habari kwenye magazeti kabla sijajua ninunue gazeti lipi. Mara navutiwa kuangalia picha kadhaa za wasanii wa filamu kwenye ukurasa wa mbele gazeti moja pendwa (la udaku) pamoja na kichwa cha habari: “Hatuibiwi... Haki ya Mungu tunaibiwa”.

Picha zinazopamba ukurasa huu wa mbele wa gazeti hili ni za baadhi ya wasanii wa kundi la Bongo Movie kwa upande mmoja zinazoambatana na neno 'Hatuibiwi', na wale walio watiifu kwa Shirikisho la Filamu Tanzania na maneno 'Haki ya Mungu tunaibiwa', kwa upande mwingine.

Aug 11, 2011

BONGO MOVIE VS TAFF: Ukimya wa Serikali kuhusu mgogoro huu unatia shaka

Katibu Mtendaji wa Basata, Ghonche Materego
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, 
Dk. Emmanuel Nchimbi
Kiongozi wa Bongo Movie, Jacob Steven (JB)

NI wazi kuwa mgawanyiko uliopo wa wasanii na wadau wa tasnia ya filamu nchini kati ya kundi la Bongo Movie Club na Shirikisho la Filamu Tanzani (TAFF), umezidi kukua huku kila kundi likipanga mbinu mbalimbali ili kulidhibiti kundi jingine. Kundi moja kwa kusaidiwa na mfadhili wao wamekuja na mpango wa kupandikiza chuki kati ya wasanii wa filamu na kiongozi wao.

Katika muda wote tangu kuanza kwa mtafaruku wa makundi haya mawili serikali imeonekana kuwa kimya pamoja na kwamba Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi, wakati fulani kukiri kuwepo matatizo ya kutoelewana kwa wasanii wa filamu hapa nchini, hali ambayo inarudisha nyuma maendeleo ya sanaa.

Aug 5, 2011

Zipi fursa za masoko ya filamu zetu nje ya nchi?

Chumo, mojawapo ya filamu za Tanzania
zilizofanikiwa katika soko la kimataifa kwa
sababu ya kuwezeshwa na taasisi za Kiserikali
na za kifedha.

 Filamu ya Men's Day Out inayotarajiwa
kutoka hivi karibuni

WIKI iliyopita nilianzisha mjadala kwa njia ya swali: “upi mfumo unaotufaa kwa ajili ya filamu zetu?”, katika mjadala huu wasomaji kadhaa wamejitokeza kuchangia mawazo yao, ingawa wengi wao wameonekana kukubaliana na hoja nilizotoa kwa asilimia mia jambo ambalo sikubaliani nalo na sikuwa nikilihitaji.

Naomba ieleweke kuwa yale niliyoyaandika ulikuwa ni mtazamo wangu binafsi ambao sidhani kama unaweza kuwa sahihi kwa asilimia mia kwa mia, kuanzisha mjadala kulikuwa na maana ya kutaka kupata hoja kinzani na mawazo mbadala yanayoweza kusaidia kuboresha soko letu. Sikuanzisha mjadala ili nisifiwe na kujaziwa pongezi kemkem.

Kampuni ya Steps yaja na mbinu chafu dhidi ya shirikisho la filamu

Jacob Steven (JB)

 Single Mtambalike (Richie)

Habari za kuaminika kutoka kwenye chanzo kimoja zimeupasha mtandao huu kuwa kampuni ya usambazaji wa filamu nchini ya Steps Entertainment imeanza kuandaa mbinu chafu kwa kuwatumia wasanii nyota ambao wapo chini ya kampuni hiyo.

Habari za kuaminika zinasema kuwa majuzi kampuni hiyo iliwatuma wasanii wawili walio chini ya Bongo Movie Club, Jacob Steven (JB) na Single Mtambalike (Richie) kwenda kuonana na Mtendaji Mkuu wa Baraza la Sanaa la taifa (Basata) ili kuweka mambo sawa.

Aug 2, 2011

JUKWAA LA SANAA: Kampuni ya usambazaji ya Steps Entertainment yalalamikiwa

 Katibu Mtendaji wa Basata, Ghonche Materego akieleza jambo

 Mwakilishi wa Bodi ya Ukaguzi wa Filamu, George Tailo

Baadhi ya washiriki wa Jukwaa la sanaa

Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), kupitia program yake ya kila wiki ya Jukwaa la Sanaa Jumatatu wiki hii imewakutanisha wasanii na Kampuni ya usambazaji wa kazi zao ya Steps Entertainment, kwa lengo la kuja na mikakati ya pamoja ya uboreshaji wa soko. 

Wakizungumza kwenye Ukumbi wa Baraza hilo, wasanii wengi walitupa lawama kwa wasambazaji hao kwa kile walichodai kwamba, wamevuruga mfumo wa usambazaji wa kazi zao hapa nchini kiasi cha kufanya wasambazaji wengine waliokuwepo kushindwa kuhimili.