KWA siku za karibuni tumekuwa na mazungumzo ya kina kati
Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania
(CTI) na taasisi zingine kuhusu mpango-mkakati wa nam,naa ya kudhibiti bidhaa
bandia na hafifu (counterfeit and substandard) zinazotishia uhai wa soko la
kazi za Kitanzania zikiwemo kazi za sanaa (filamu na muziki).
Siku hizi imekuwa si jambo la ajabu kusikia au kushuhudia
bidhaa kama nondo za ubora hafifu, betri, TV,
mafeni, breki za gari, dawa nk. Jambo hili limekuwa likituumiza mno na sasa
tumelishuhudia kwa kasi likivamia sekta ya sanaa kwa kiwango kikubwa na
kutishia uhai wa soko la filamu na muziki, hasa kwenye bidhaa kama DVDs, CDs,
Tape, Vifungashio (Packaging system) nk, ambazo zinahusiana moja kwa moja na
sanaa la filamu. Inaudhi mno pale unaponunua sinema (DVD) unayotegemea kwenda
kuangalia nyumbani lakini unapoiweka kwenye deki unaitazama mara moja tu,
ukiirudia unagundua kuwa inakwama, na wakati mwingine hugoma hata kabla
haijaangaliwa!