KWA siku za karibuni tumekuwa na mazungumzo ya kina kati
Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania
(CTI) na taasisi zingine kuhusu mpango-mkakati wa nam,naa ya kudhibiti bidhaa
bandia na hafifu (counterfeit and substandard) zinazotishia uhai wa soko la
kazi za Kitanzania zikiwemo kazi za sanaa (filamu na muziki).
Siku hizi imekuwa si jambo la ajabu kusikia au kushuhudia
bidhaa kama nondo za ubora hafifu, betri, TV,
mafeni, breki za gari, dawa nk. Jambo hili limekuwa likituumiza mno na sasa
tumelishuhudia kwa kasi likivamia sekta ya sanaa kwa kiwango kikubwa na
kutishia uhai wa soko la filamu na muziki, hasa kwenye bidhaa kama DVDs, CDs,
Tape, Vifungashio (Packaging system) nk, ambazo zinahusiana moja kwa moja na
sanaa la filamu. Inaudhi mno pale unaponunua sinema (DVD) unayotegemea kwenda
kuangalia nyumbani lakini unapoiweka kwenye deki unaitazama mara moja tu,
ukiirudia unagundua kuwa inakwama, na wakati mwingine hugoma hata kabla
haijaangaliwa!
Tape ndogo (Min div) zinazotumika kwenye kamera kwa ajili ya
kuchukulia picha nyingi ni bandia, na hata vifungashio si imara kabisa. Huu mpango-mkakati
unalenga kutafuta wataalam wa kusaidia kugunduaa bidhaa bandia kwani kuna
tishio la kuja kukosa maktaba za kazi zetu siku za baadaye, kwa kuwa kazi zote (DVD
na CD) zitakuwa hazichezi (zinagoma kuonesha).
Hili ni jambo zuri sana kwa mustakabali
wa soko la kazi zetu, lakini bado tunatindikiwa na jambo moja muhimu sana katika kudhibiti kiwango
hafifu, jambo hili ni maudhui katika hadithi zetu, kwani nayo yanaonekana
kukosa viwango vinavyotakiwa.
Kwa miaka kadhaa, sekta ya filamu Tanzania imeshuhudia utofauti
mkubwa kati ya maudhui katika hadithi zetu na kile watazamaji wanachokihitaji,
na matokeo yake yameendelea kuyumbisha mikakati ya soko na sera za usambazaji.
Maudhui lazima yahusishwe moja kwa moja na mahitaji ya watazamaji ili kuwe na nafasi
ya mafanikio kwenye soko.
Maudhui yanayofaa katika kizazi cha leo ni yale yanayokwenda
sambamba na watazamaji ndani ya akili zao na kuihusisha jamii moja kwa moja.
Mafanikio yanayotokana na maudhui yanategemea sana mmenyuko wa watazamaji, na
kujenga maudhui yaliyo kwenye mstari na mwelekeo wa watazamaji na matarajio yao
imekuwa vigumu, na sasa inahitajika kwa watayarishaji/ waandishi wa miongozo ya
filamu kujihusisha moja kwa moja na mtazamo wa watazamaji katika mazingira
waliyomo. Kwa matokeo haya, utafiti ni suala la kupewa umuhimu mkubwa kabla ya
kuandaa kazi husika.
Kitu ambacho mtayarishaji/ mwandishi anapaswa kujua kuhusu watazamaji wake ni muhimu
Kundi la kwanza la watazamaji wa filamu ni la akina mama wa nyumbani, wafanyakazi wa ndani, na vijana wasio na ajira. Kundi la pili ni la watazamaji linalotokana na matokeo ya moja kwa moja ya kituo cha
Na bila shaka kuna kundi la tatu linalotokana na watazamaji
Watanzania walio nje ya nchi na Waafrika (hasa wanaojua au kukipenda Kiswahili)
katika bara la Afrika na maeneo waliko. Ni muhimu kuelewa kwamba kila moja ya
makundi haya ya watazamaji yana muundo na mawazo ambayo ni tofauti sana na kundi jingine.
Utafiti nilioufanya kwa miaka mitatu unaonesha kwamba
watazamaji wa filamu za Kitanzania wamegawanyika kama
ifuatavyo:
Asilimia 67 ya watazamaji wa filamu hizi wanaishi ndani ya
Tanzania, asilimia 25 wanatoka katika nchi nyingine za Afrika Mashariki, na
asilimia 8 wanatoka sehemu zilizobaki za dunia, hasa ambako Kiswahili
kinafundishwa au kupewa umuhimu.
Pia ni asilimia 30 ya wakazi wanaoishi mijini ndiyo
huangalia filamu za Kitanzania. Takwimu hii inatofautishwa kulingana na umri:
Asilimia 50 ya watazamaji hawa ni wenye umri kati ya miaka 10-24, asilimia 30
ni wenye umri kati ya miaka 25-34, asilimia 15 ni kati ya watu wenye umri wa
miaka 35-49 na asilimia 5 tu ya watu wenye umri zaidi ya miaka 50 ndiyo
huangalia filamu hizi. Dar es Salaam ndiyo mji unaoongoza kuwa na idadi kubwa
ya watazamaji wa filamu ikichukua asilimia 31. Hata hivyo, vijana wadogo ndiyo
wenye mazoea ya kwenda kwenye mabanda ya video.
Katika utazamaji filamu hizi, kuna dhana ambayo huendana na
mitazamo ya watazamaji (matamanio, maadili, na mtazamo wa mtu binafsi kulingana
na uzoefu wake katika kuangalia kazi mbalimbali) na vitu hivi huathiri namna
watazamaji wanavyohusiana na dunia inayowazunguka, ikiwa ni pamoja na maudhui.
Kabla hadithi yako haijawafikia watazamaji, tayari mtazamaji
atakuwa na picha ya kipi anataka kukiamini na kama
hadithi yako imeandaliwa katika mtazamo mzuri, mtu wa aina hiyo huamini na
hununua kazi bila kusita. Kama hadithi
itaifikia jamii ya watazamaji ambao mtazamo wao utalingana na kisa chako, wigo
wake utapanuka, watu watapeana taarifa kwa njia ya neno kwa neno (ambayo ni
njia ya ufanisi zaidi kwa mkakati wa soko) na hujenga nidhamu ya utazamaji wa
filamu.
Hakuna hadithi inayofanikiwa kama watazamaji hawapati kitu
wanachokiamini - na kwa wastani wa filamu 100 za Kitanzania, watazamaji wetu hawataweza
na wala hawataona kila kitu wanachohitaji, watachukua na kuchagua kati ya
filamu nyingi wanazoziona ili kuridhisha matakwa yao .
Maudhui yanayokubalika sana
ni yale yanayosimulia jambo linalofahamika zaidi kwa watazamaji. Hii inaweza
kupimwa kwa njia mbalimbali, wengi hasa, utafiti wa msingi unaweza kutusaidia
kutambua aina ya hadithi tunazohitaji kuwaambia walengwa, aina ya wahusika
tunaowahitaji kutusaidia kwenye hadithi zetu, aina ya watazamaji tunaowahitaji
kuwaambia hadithi zetu, na majukwaa sahihi kwa ajili ya kusambaza hadithi zetu.
Kuwaelewa watazamaji ni hatua moja muhimu
Pamoja na ukamilifu wa filamu katika usambazaji mara kwa
mara, watazamaji kwa urahisi wanaweza kujiendekeza katika mitazamo yao (indulge their
worldviews); wakapuuza kazi ambayo haiwaakisi wao moja kwa moja.
Kuandaa hadithi iendane na ladha ya watazamaji - hasa kwa
kuelewa kuwa watazamaji hawataki kubadilishwa mitazamo yao ,
wanataka kuimarisha mitazamo yao
(they want it to be reinforced) - itakusaidia kuanzisha mijadala kuhusu masuala
muhimu kwa watazamaji wako.
Vizuri tu kama ,
utaambatanisha ubora wa kiufundi wa filamu yako uendane na ubora wa watazamaji
wako waliouzoea. Hutoweza kufanya biashara - kwa mfano, kuwapa filamu yenye
ubora hafifu (low quality film) watazamaji ambao wamezoea kuangalia sinema za
kigeni, ambazo zimetengenezwa kwenye
tasnia za filamu zilizoendelea zaidi kwa kiwango cha juu cha ubora.
Alamsiki…
No comments:
Post a Comment