Prof. Amandina Lihamba akiongea kwenye Jukwaa la Sanaa,
kushoto ni Katibu Mtendaji wa Basata, Gonche Materego
Idara ya Sanaa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
ambapo ni chimbuko la wasomi katika sanaa
Nembo ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
wanapotoka wasomi wa kada mbalimbali
Amandina Lihamba na marehemu Kaduma
kwenye sinema ya Harusi ya Mariam
Jukwaa la Sanaa la Baraza la Taifa la Sanaa la Taifa
linalofanyika kila Jumatatu limekuwa kiungo muhimu kwa wadau mbalimbali wa
sanaa hapa nchini, Jumatatu hii ya tarehe 17 Januari, 2011 Jukwaa hilo
lilishuhudia wasomi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na waigizaji mahiri
katika tasnia ya filamu Tanzania wakijadili kuhusu mustakabali wa Tasnia ya
Filamu Tanzania chini ya uratibu wa Profesa Amandina Lihamba.
Monalisa akiwa kashika tuzo aliyoipata ZIFF
Single Mtambalike (Richie)
Katika Jukwaa la Sanaa siku hiyo kuliendeshwa darasa kwa pande zote mbili, wasanii waliongozwa na Yvonne Cheryl maarufu kama Monalisa na Single Mtambalike maaruf kama Rich Richie huku upande wa Chuo Kikuu ukiongozwa na Prof. Amandina Lihamba na Dk. Mona Mwakalinga.
Dk. Mwakalinga alielezea kuhusu historia ya filamu Tanzania na kubainisha kuwa ni nchi ya kwanza Kusini mwa Jangwa la Sahara ukiitoa Afrika Kusini, filamu kwanza iliyotengenezwa Tanzania ilitolewa mwaka 1935 kwa nakala 35
No comments:
Post a Comment