Sehemu ya jiji la Dar es Salaam
ilipofanyika semina ya wadau wa filamu
Prof. Martin Mhando
Semina iliyowakutanisha wasanii na wadau mbalimbali wa filamu iliyofanyika Ijumaa tarehe 14 Januari kwenye ukumbi wa Kituo cha Utamaduni cha Ufaransa (Alliance Francaise), pamoja na mambo mengine kulikuwa na ushari kwa Wasanii na wadau hao kuunda kundi la ushawishi serikalini ili kuitambulisha serikali umuhimu wa sanaa ya filamu pamoja na muziki.
Ushauri huo wa kuwataka wadau kuunda kundi la ushawishi umetolewa na wataalamu wa mambo ya filamu na sanaa kwa ujumla wakati wa semina hiyo iliyohusu umuhimu wa utamaduni na uchumi kupitia filamu.
Habari zaidi zinaelezea kuwa kundi hili litatakiwa kuitambulisha tasnia ya filamu kwa Wabunge na Serikali ili waone umuhimu wa sekta hii na kuangalia suala la uharamia wa kazi za sanaa na kuwasaidia kupigana na wizi huo kwa kushiriki kutunga sheria kali au kutoa hoja kuhusu tatizo hili.

Wengi wanaamini kuwa sekta ya filamu imesahaulika kutokana na sheria ya filamu ya mwaka 1976 namba 4 kutofanyiwa marekebisho kwa miaka mingi na wala hakuna yeyote anayeonekana kuguswa na jambo hili.
No comments:
Post a Comment