Kipindi hiki kinachohitajika
sana kimekuwa kikiimarika katika bara Afrika. Mapema mwaka huu kulikuwa na
uzinduzi wa Netflix katika soko la Afrika, hatua iliyofurahisha wateja wengi. Hatua
hii inajiri wakati ambapo Showmax cha Afrika Kusini kinatarajiwa kuingia katika
soko la Kenya. Mipango mengine ni ile ya ushirikiano wa kati ya Airtel na
Ericsson kuzindua huduma kwa jina NUVU.
NUVU ilianzishwa nchini
Nigeria, hivyo, kuwasaidia wateja kuwa na uwezo wa kuona filamu 3000 za
nyumbani na hata kimataifa. Safaricom pia ilikuwa na hamu ya kuanzisha mtandao
wa video ikishirikiana na kampuni moja ya India, ‘VuClip’, kuwapatia wateja
uwezo wa kuona video katika simu zao kwa shilingi 10 pekee.
Hata hivyo kampuni iliyopata
ufanisi mkubwa ni ile ya Buni TV ambayo hutoa video. Mwaka 2012 Buni ilianzisha
Video zake na baada ya miezi tisa ilifanikiwa kupata takriban wateja milioni
moja. Trace TV sasa imetangaza kwamba inaimiliki Buni TV kama mpango wake wa
kuzindua video yake kwa jina Trace Play.
Katika makubaliano hayo,Trace
TV imefanikiwa kumiliki haki za runinga na VOD ya vipindi vyote vya Buni
vikiwemo ‘Ogas at the top’ nchini Nigeria na XYZ nchini Kenya inayotayarishwa
na kampuni mwenza ya Buni Media.
Buni TV ilianzishwa na mchoraji vibonzo, Godfrey
Mwampembwa, maarufu kwa jina la Gado, ambaye ndiyo mwenyekiti wake. Kampuni
hiyo ilikuwa imewaajiri watu 88 wakati ilipouzwa.
No comments:
Post a Comment