Ramani inayoonesha nchi za SADC |
MAPEMA Machi mwaka huu kuliandaliwa Tamasha la Kusherehekea Wanawake wa
SADC Katika Sanaa ya Maigizo na Dansi lililofanyika mjini Johannesburg.
Wanawake wa Zambia katika kikundi cha dansi walitumia
michezo ya maigizo kwa ajili ya maendeleo kwa kuhamasisha wanakijiji kupanda
zaidi ya miti 5,000 na kujenga majengo matatu ya madarasa kwa kipindi cha miaka
mitatu katika Jimbo la Kusini mwa Zambia.
Tamasha hilo liliandaliwa na "Southern Africa Theatre Initiatives (SATI)" na lilikuwa na lengo la kuonesha jukumu la wanasanaa wanawake wa nchi za SADC kuungana na kuleta mabadiliko katika kanda.
“Wanasanaa wanawake wanapuuzwa pamoja na kazi
kubwa wanayofanya kuunganisha na kuendeleza jumuiya. Wanachohitaji ni kutambua
na kupatiwa msaada tu,” alisema Mpo Molepo, katibu wa SATI.
Mwaka 2002, kundi la sanaa la Kamoto Community lilibainisha
ukataji wa miti kama tatizo kuu katika Jimbo la Kusini mwa Zambia na hali mbaya
ya madarasa kama jambo linaloathiri wanafunzi katika Shule ya Msingi Chiyumu.
"Kupitia mchezo wetu tulipata fedha kwa ajili
ya ujenzi wa majengo ya madarasa katika Shule ya Msingi Chiyumu ambayo baadaye
tuliyakabidhi kwa serikali," alisema mkurugenzi wa kundi la sanaa la Kamoto
Community, Mary Manzole Kamoto.
“Kwa suala la mabadiliko ya tabia nchi, kuna
ukataji mkubwa wa miti unaoendelea na tulikuwa tukifanya maigizo kuhamasisha
watu kupanda miti. Baada ya mchezo wetu, Walianza kupanda miti na hii ilibadili
mwenendo wa mvua katika jimbo zima.
"Hii ilibadili mwenendo mzima wa kilimo katika jimbo ambalo kwa miaka mingi lilikuwa likinunua mahindi kutoka majimbo mengine na sasa linauza mahindi," alielezea Jean Shamende, mwanachama wa kikundi hicho.
"Hii ilibadili mwenendo mzima wa kilimo katika jimbo ambalo kwa miaka mingi lilikuwa likinunua mahindi kutoka majimbo mengine na sasa linauza mahindi," alielezea Jean Shamende, mwanachama wa kikundi hicho.
Ghetto Artists, kundi jingine la wanawake vijana kutoka
nchini Botswana, liliwasilisha moja ya maigizo yake, “Strength of A Woman”
wakati wa tamasha hilo. Mchezo huo unaonesha maisha ya hatari na halisi ya
unyanyasaji dhidi ya vijana wa kike.
“Tunaona mabadiliko chanya ya mchezo huu (nchini
Botswana); wasichana walionyanyaswa wanajitokeza, baadhi wanatafuta huduma za
ushauri nasaha na wazazi na wanaume wanakiri. Vijana wa kike na kiume wanarejea
mashuleni kupitia mchezo huu,” alisema mkurugenzi, Saone Bokitshane.
Aliongeza: “Sanaa ina nguvu kubwa. Kupitia sanaa, unaweza kuponya watu na kupitia sanaa unaweza kuelimisha jumuiya mzima na kujenga upya nchi.
Aliongeza: “Sanaa ina nguvu kubwa. Kupitia sanaa, unaweza kuponya watu na kupitia sanaa unaweza kuelimisha jumuiya mzima na kujenga upya nchi.
“Ni wakati muafaka serikali zetu zinafadhili
wanasanaa wa kike kutengeneza michezo ya VVU/UKIMWI. Kupitia michezo ya
wanawake tunaweza kukomesha kuenea kwa gonjwa hilo.”
Na kutoka Zimbabwe kulikuwa na 'Ebony and Ivory',
kuhusu wanawake wawili na mabadiliko ya haraka ya moyoni na maumivu
yaliyosababishwa na vita, ghasia na utesaji.
Pia ilioneshwa michezo na dansi lililoonesha maisha ya wanawake nchini Lesotho na Afrika Kusini.
Pia ilioneshwa michezo na dansi lililoonesha maisha ya wanawake nchini Lesotho na Afrika Kusini.
Kwa kweli tamasha hilo lilitoa fursa ya kuonesha
masaibu yanayoathiri wanasanaa wanawake, ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa
usawa wa kijinsia katika sekta ya sanaa.
Kwa mujibu wa na chama cha haki za wanasanaa
kijulikanacho kama ‘Artists’ Rights Union’, ni asilimia tano tu ya watengenezaji
michezo hiyo ni wanawake.
Tamasha hilo lilitokana na utafiti uliofadhiliwa
na SATI nchini Afrika Kusini, Malawi, Namibia, Zimbabwe, Zambia, Mauritius,
Swaziland, Shelisheli, Msumbiji, Tanzania, na Lesotho.
Prof Amandina Lihamba (Kwa hisani ya shereheyetu blog) |
Utafiti wa mwigizaji na mwanazuoni wa Tanzania,
Profesa Amandina Lihamba, ulitaka kujua kama sauti za wanawake zilisikika kiasi
cha kutosha katika duru za sanaa na fasihi Kusini mwa Afrika.
Mbali na tamasha hili, nchi za kusini mwa Afrika
zina makubaliano miongoni mwa wadau na wachunguzi wa tasnia filamu na
televisheni, kwamba, utajiri uliopo wa ubunifu miongoni mwa vijana na hadithi
zilizopo katika ukanda huu vitumike vyema.
Hata hivyo, wote wanakubaliana kwamba tasnia ya
filamu katika nchi hizi bado iko chini sana na, katika hali halisi, inazidi
kushuka.
Utafiti unaonesha kuwa tasnia ya filamu ya nchi za
SADC ni ndogo na haijapiga hatua, ingawa inaonekana kutoa fursa nyingi katika
kuendeleza miundombinu na hadithi zetu.
Kampuni nyingi katika sekta ya filamu na
televisheni ni ndogo ndogo na zinazoonekana kuchangia katika ajira na ukuaji wa
uchumi, na matatizo ya kupata fedha za kutengenezea filamu ni
moja ya kikwazo kikubwa kwenye maendeleo ya sekta ya filamu na televisheni
katika nchi hizi.
Katika nchi za SADC, ukiacha Afrika Kusini, haziwezi
kujisema kuwa zina tasnia ya filamu, ila zina malighafi za filamu.
Afrika Kusini inaonekana kuwa nchi pekee katika nchi
za SADC ambayo uwekezaji kutoka sekta binafsi (kinyume na ufadhili) kwa ajili
ya uzalishaji filamu unapatikana bila matatizo.
Miundombinu maalumu katika filamu inaiwezesha nchi
ya Afrika Kusini kutengeneza filamu bora za kiwango cha kimataifa. Hali hii,
ukichanganya na maeneo yake mbalimbali na hali nzuri ya hewa imeifanya Afrika
Kusini kuwa eneo maarufu la kutengenezea filamu.
Katika muktadha wa kidunia, hali hii inayafanya
maeneo ya Afrika Kusini, Mauritius na Namibia kuwa maeneo muhimu na yenye
gharama ndogo za kutengenezea filamu katika nchi za SADC.
Changamoto kubwa inazozikumba tasnia za filamu katika
nchi za SADC ni ukosefu wa uwekezaji katika sekta binafsi ambazo zingeweza
kutoa fedha za utengenezaji wa filamu bora kwa soko la nje.
Umiliki wa vipindi kwa vyombo vya utangazaji na
tabia ya uvivu wa kufikiri katika kubuni kwenye tasnia ya filamu katika
kuhakikisha maendeleo ya mipango ya kuuza nje inaendelea kuikwaza tasnia hii.
Hata hivyo, nchi za Kusini mwa Afrika zina kiwango
kizuri cha miundombinu ya utengenezaji wa filamu na vipindi vya televisheni
ukilinganisha na nchi zingine za Afrika nje ya ukanda huu.
Miundombinu hii ni pamoja na vitendea kazi vya
uzalishaji na uhariri, vitenda kazi vya kutolea mafunzo na vifaa, ingawa filamu
zinazozalishwa kutoka nchi za Afrika Magharibi mara nyingi zinachukuliwa kama
filamu bora kuliko zinazozalishwa na nchi za SADC.
No comments:
Post a Comment