![]() |
Ramani inayoonesha nchi za SADC |
MAPEMA Machi mwaka huu kuliandaliwa Tamasha la Kusherehekea Wanawake wa
SADC Katika Sanaa ya Maigizo na Dansi lililofanyika mjini Johannesburg.
Wanawake wa Zambia katika kikundi cha dansi walitumia
michezo ya maigizo kwa ajili ya maendeleo kwa kuhamasisha wanakijiji kupanda
zaidi ya miti 5,000 na kujenga majengo matatu ya madarasa kwa kipindi cha miaka
mitatu katika Jimbo la Kusini mwa Zambia.
Tamasha hilo liliandaliwa na "Southern Africa Theatre Initiatives (SATI)" na lilikuwa na lengo la kuonesha jukumu la wanasanaa wanawake wa nchi za SADC kuungana na kuleta mabadiliko katika kanda.
“Wanasanaa wanawake wanapuuzwa pamoja na kazi
kubwa wanayofanya kuunganisha na kuendeleza jumuiya. Wanachohitaji ni kutambua
na kupatiwa msaada tu,” alisema Mpo Molepo, katibu wa SATI.