Mmoja wa waigizaji maaruf wa sinema za Hollywood, Angelina Jolie |
Ripoti moja ya utafiti wa
kwanza kufanyika duniani kuhusu wahusika wa kike katika filamu, umebainisha
kuwa ubaguzi wa wanawake na wasichana umeenea mno katika sekta hiyo ya filamu. Ripoti
hiyo iliyozinduliwa mwezi Septemba mwaka jana imetokana na utafiti
ulioidhinishwa na taasisi ya Geena Davis kuhusu Jinsia katika vyombo vya
habari, ikisaidiwa na Shirika linalohusika na masuala ya wanawake, UN Women,
pamoja na Wakfu wa Rockefeller.
Utafiti huo ulifanywa na Stacy
L. Smith (PhD) na timu yake ya watafiti kutoka Chuo cha Mawasiliano cha Annenberg,
Chuo Kikuu cha Southern California. Utafiti huo ulitathmini filamu maarufu
kutoka nchi ambako sekta ya filamu imepiga hatua zaidi, zikiwemo Australia,
Brazil, China, Ufaransa, Ujerumani, India, Japan, Urusi, Korea Kusini,
Marekani, Uingereza, pamoja na ushirkiano unaofanywa kati ya Uingereza na
Marekani.
Huku wanawake wakiwa
wanawakilisha zaidi ya nusu ya idadi nzima ya watu duniani, wahusika wa kike
wanaoongea katika filamu hizo ni chini ya theluthi moja. Wahusika wa kike
wanaoonekana kwenye runinga ni chini ya robo ya wahusika wote, yaani asilimia
22.5.
Utafiti unaonesha pia kuwa,
wanapotumiwa, wanawake hawapewi nafasi za uwezo mkubwa, na wanawakilisha chini
ya asilimia 15 ya wakuu katika biashara, wanasiasa, wanasayansi na teknolojia,
wahandisi na wanahisabati.
No comments:
Post a Comment