Rais Jakaya Mrisho Kikwete na marehemu Steven Kanumba |
KUMEKUWEPO
mjadala kama hali ya sasa katika soko la filamu linaweza kuitwa ‘sekta rasmi’
ambapo mitaji, mitambo na rasilimali zipo kila mahali. Hakuna maendeleo yoyote
yatakayopatikana pasipo uwepo wa Sera ya Filamu. Sera ya Filamu ni hati nzuri
inayoandaa mazingira mazuri kwa ajili ya uzalishaji wa filamu na masoko.
Ni hati
kuhusu hadhi na thamani ya sekta inayoonesha kutokosekana kwa miongozo ya
lazima na visheni, inayotambua kuwa Filamu ni njia ya kipekee ya mawasiliano,
ni njia ya kuelimisha na kuburudisha, inayotuweka pamoja, kupashana habari na
kuhamasishana.
Zaidi kuliko
njia nyingine yoyote ya mawasiliano ya umma, filamu inaweza kutumika kama
chombo cha kuendeleza mabadiliko chanya ya kijamii pamoja na kuimarisha na
kujenga uhusiano mpya kati ya utamaduni na maendeleo ya Taifa. Filamu ni njia
mtambuka ya mawasiliano ya kiutamaduni ambayo ni muhimu inayoweza kutumiwa na
Tanzania kuionesha dunia rangi yake halisi.
Kwa hiyo ni
dhahiri kwamba akili zinazoweka pamoja sera zinakwenda na wakati na zina maono.
Hata hivyo, hali ya sasa inaonekana kutoendana na hisia zinazojionesha. Hali ya
utengenezaji wa filamu inahitaji kuchukuliwa kwa tahadhari kubwa.
Katika suala
la teknolojia ya utayarishaji wa filamu nchi kwa sasa inarudi nyuma haraka na
inaoza. Utamaduni wa kuangalia filamu za kigeni uliojengwa kwa miaka mingi umekufa
na kuzaliwa itamaduni wa uangaliaji wa filamu za ndani lakini zikiwa katika
maudhui ambayo bado kwa kiasi kikubwa yapo katika dhana za kigeni.
Kwa vyovyote
ilivyo, nchi hii inaonekana kujifunga, azimio ambalo, linahitaji jitihada za
pamoja za mapinduzi ya kiutamaduni yatakayothaminiwa kwa teknolojia iliyopo na
ya bei nafuu.
Inaweza
isiwe muhimu sana kushiriki katika mapitio ya Sera ya Filamu au hata
miundombinu isiyokuwepo au fedha za kujikimu na utaratibu wa mitaji ya fedha za
uzalishaji filamu nchini kama itafanywa kuwa mada tofauti. Kwa kweli, inahitaji
semina ya siku nzima kutathmini fedha na masoko ya filamu nchini. Kukosekana kwa sera kumezifanya filamu zetu kuwa kama
mchezo wa soka bila refa, mkutano bila mwenyekiti, darasa bila mwalimu, au
familia bila mzazi.
Sinema
nyingi (zaidi ya asilimia 90) zina upungufu mkubwa katika ustaarabu wa kisanii
(artistic sophistication) unaotarajiwa katika levo ya kimataifa. Lakini pia ni
dhahiri kwa watazamaji wa ndani wanaonekana kutokuwa na mbadala na hivyo
kulazimika kuendelea kutazama filamu hizi japo shingo upande. Ili sekta ya
filamu ikue na kufika kiwango cha kimataifa ni lazima kuwe na uwekezaji mkubwa
unaofanyika. Suala lililopo ni wapi fedha hizo zitatoka na nini kitaongeza
ubora au hata uwezekano wa “ideology” ya filamu zinazotayarishwa. Pesa
hazipatikani bure, lakini sinema zinapaswa, jambo ambalo ni ukweli kinzani (paradox)
wa sekta ya filamu katika jamii ya kibepari.
Ushiriki
mchache na wa mbali kati ya Benki na soko la mitaji ni ushahidi wa kutosha wa
utaratibu wa kizamani wa misaada ya fedha katika dunia ya sasa. Inatosha
kusema, kiwango cha ushiriki wa misaada ya fedha katika sekta yoyote ikiwa ni
pamoja na kuchukua tahadhari ya mfumo kuamua ukuaji wa uchumi, uhimili na ubora
wa bidhaa unaoshindwa kuongeza uzalishaji.
Wakati
huohuo, kama msingi mkuu ni dhaifu, haiwezekani kusema rasilimali watu
zinapatikana kwenye sekta ya filamu (ikumbukwe kuwa sisi bado ni sekta ndogo tu)
isiyo na tija. Kuna waandishi wa skripti, watayarishaji, waongozaji, na
wataalamu wengine, ambao wanaweza kupambana na changamoto ya miongozo yoyote
bila kujali ugumu.
Jambo moja ambalo
linaonekana kwa haraka lipo kati ya rasilimali watu ni tofauti na elimu ya
asili. Kwa hiyo inapaswa kuangalia kuwa elimu bora ya filamu inapatikana katika
nchi. Je, kuna mwelekeo wa wazi na kiwango na ushawishi wa utamaduni katika
mafunzo? Katika hati ya Sera ya Filamu, ni lazima iwepo sehemu inayohusika na
mafunzo, utafiti na maendeleo.
Elimu ya
filamu ni jambo muhimu sana kwetu (au taifa jingine lolote) kuhadithia hadithi
zetu na kuionesha Tanzania kama inavyotakiwa kujulikana kwa mataifa mengine,
bila ya kuwa na tatizo tunalolishudia la watengeneza filamu wa kigeni
wanaowakilisha taifa/bara isivyo sahihi au kukosa pointi muhimu za
kihistoria/masimulizi ya kisiasa (filamu za kisiasa ni kama: ‘Hotel Rwanda’,
‘Blood Diamond’, ‘Sometimes in April’ na ‘The Last King of Scotland’,
zilizotengenezwa kwenye bara hili na watengenezaji filamu wa kigeni).
Tunachoweza
kuzingatia kwa sasa ni jinsi ya kuifanya elimu inayopatikana katika shule za
filamu (zitakazokuwepo) iweze kutumiwa kutokana na hali yetu ya sasa ambapo
hakuna tena busara ya kiuchumi kwa kuwekeza katika hisa za filamu (film stock).
Mitaala ya Taasisi zinazofundisha filamu lazima ijumuishe pamoja na jinsi ya
kupenyeza vyote teknolojia na utamaduni wa kuzalisha kazi za viwango vya
kimataifa katika masuala ya ubora wa maudhui yanayowasilishwa.
Pia tunapaswa
kuipitia upya Sheria ya Filamu Na. 4 ya 1976 ambayo haifafanui wala kuweka
mifumo yoyote ambayo inaweza kutoa majibu ya maswali yaliyopo. Sheria hii inazungumzia
tu kuhusu uanzishwaji wa taasisi ya filamu (Bodi ya Ukaguzi wa Filamu na Michezo
ya Kuigiza) ambayo hata hivyo imenyimwa mamlaka kamili, kwani inafanya kazi
kama taasisi ya kusimamia maadili na kupanga madaraja tu.
Filamu kama
dhana nzima haiwezi kubishaniwa, kinachoweza kujadiliwa ni uwezekano zaidi wa
kutatuliwa kwa dhahania (subjectivity) ya uzuri ulio katika jicho la mtazamaji.
Sababu inayoshawishi
uzalishaji wa filamu nchini kama ilivyo katika nchi nyingine ni maudhui ya
filamu yanayoweza kuamuliwa na sababu kubwa ya kuwa utamaduni wa watu na mbinu
zao zinapelekea nchi kuwa katika hali ya utulivu. Pia kuna muingiliano
(uhusiano) wa uchumi, matarajio na muingiliano wa kijamii wenye jukumu kubwa
katika kuamua utamaduni wa filamu. Ni kama jamii inapata aina fulani ya
wafanyakazi inaostahili, watengeneza filamu kupitia utafiti huamua nini soko linataka
katika masuala ya dhamira, hata hivyo bado ‘kinachowasilishwa’ huamuliwa na mtayarishaji
na muongozaji.
Bado kilicho
katikati ya vikosi vya kimasoko na watu wakati mwingine ni nafasi isiyopendeza ya
wakosoaji wa filamu, kwa ambaye ana wajibu wa kufanya vizuri.
Hali ya
kiuchumi na kisiasa bado ni ya kiwango cha chini sana. Kuna upuuzwaji mkubwa wa
sekta hii, serikali badala ya kuitazama sekta hii kibiashara na chanzo muhimu
cha kichumi (new sector with economic potential) wanaichukulia kama sehemu ya
burudani. Bado imekuwa haipewi kipaumbele japo imeonekana kuchangia kwa kiasi
kikubwa katika ajira na pato la Taifa. Kwa sababu hiyo sidhani kama tunaweza kuweka
imani yetu kwa serikali iliyopo kutuunga mkono. Hii inaweza kuwa sababu ya kushindwa
kwetu, na mimi sina uhakika wa uwepo wa hali hii, ambapo inaweza kuwa ya
manufaa kwa baadhi ya mipango ya filamu kufanyika nchini.
Tanzania
ni moja ya nchi chache zenye maeneo mazuri ya kuvutia yanayofaa kabisa kwa
kutengenezea filamu, ni nchi yenye wasanii wengi wazuri wenye vipaji lakini
waliokosa muongozo.
Sisemi kuwa
nina ufahamu wa hali ya kiwango kikubwa zaidi, lakini nina shauku ya kujua iwapo
itawezekana kuona serikali ikija na mpango madhubuti wa kuandaa na kuwapa elimu
na teknolojia inayohitajika watayarishaji, waongozaji na watendaji wengine wa
filamu nchini. Hii itaonekana kuwa tumekuja na mpango wenye manufaa makubwa
ikiwa itawezekana.
Nawasilisha.
No comments:
Post a Comment