![]() |
Sanaa za Tanzania
|
KATIKA ulimwengu wa kimaada unaodhibitiwa na
fikra za kupenda dunia, thamani za utamaduni (sanaa ikiwemo ndani yake) huwa
hazipewi nafasi na siku zote utajiri wote wa sanaa unapimwa kwa fedha.
Suala muhimu katika ulimwengu huo ni fedha,
kwa hivyo kila kitu kinapimwa thamani yake kwa kuangalia kitaingiza kiasi gani
cha fedha.
Utaona inatazamwa elimu fulani itaingiza fedha
kiasi gani, inaangaliwa kazi fulani ina uwezo wa kuingiza kiasi gani cha fedha
na vitu kama hivi. Lakini hali haiko hivyo katika upande wa utamaduni.
Hapana, kwani elimu ni njia ya kuwa na maisha
bora, na sanaa ni chombo cha kuwa na ustawi katika maisha.