Benson Wanjau Karira maarufu kama Mzee Ojwang Hatari |
Muigizaji mkongwe wa
vichekesho nchini Kenya, Benson Wanjau Karira maarufu kama Mzee Ojwang Hatari, amefariki dunia
siku ya Jumapili usiku katika Hospitali ya Taifa ya Kenyatta alipokuwa
amelazwa.
Mzee Ojwang wakati akichukuliwa vipimo vya macho |
Mzee Ojwang alikuwa amelazwa katika hospitali hiyo
akisumbuliwa na maradhi ya homa ya mapafu (Pneumonia). Muigizaji huyo ambaye
alikuwa kinara katika vipindi vya Vitimbi, Vioja Mahakamanii, Vituko na
Kinyonga, pamoja na kazi nyingine, alikuwa hajaonekana kwenye televisheni kwa
muda mrefu.
Gwiji huyo wa vichekesho ambaye alikuwa mmoja wa wachekeshaji maarufu sana wa Kenya, awali alilazwa katika hospitali ya Loresho katikati ya mwezi
Machi wakati akitibiwa tatizo la kupoteza uwezo wa kuona.
Machi 10 mwaka huu, Kikundi
cha Vitimbi kikiongozwa na Mary Khavere maarufu kama Mama Kayai, kilimtembelea Meya wa Nairobi, Mike
Sonko, ofisini kwake kuomba msaada katika kumhudumia Mzee Ojwang hospitalini.
Ugonjwa wake uliifanya
serikali kujitokeza kulipa gharama zake za matibabu huku Waziri wa Habari, Fred
Matiagi, akisema serikali itaangalia maslahi ya Kikundi cha Vitimbi.
Mzee Ojwang alisoma katika
Shule ya Misheni ya Kanisa la Pumwani ambapo alifanya mtihani wake mwaka 1952. Baadaye
alijiunga na masomo ya juu katika Shule ya Kagumo.
Kwa miaka 35, Mzee Ojwang Hatari alikuwa akiigiza vichekesho katika televisheni yaa Kenya, KBC.
Kwa mara ya kwanza alijiunga na sekta ya filamu alipokuwa na miaka 34. Ilikuwa katika miaka ya 1970 na alikuwa ndo kwanza amemaliza shule na kuanza kazi katika duka. Aliacha kazi na kujiunga na Hospitali ya Mater kama fundi msanifu (technician) lakini baada ya miaka minne alijikuta akijiingiza kwenye masuala ya burudani, hivyo kuutumia muda wake wa mapumziko kufanya maigizo.
Mwaka 2009, wasanii wa Vitimbi walipewa tuzo wakati wa uzinduzi wa Tuzo za Kalasha. Mwaka uliotangulia, Mzee Ojwang alikuwa ametambuliwa na Wakenya kama mchekeshaji aliyeaminika zaidi miongoni mwa wachekeshaji nchini Kenya.

Mzee Ojwang aliwahi kubainisha kuwa anapenda fani ya uigizaji, na ataendelea kuigiza katika maisha yake yote. Alioa na alikuwa na watoto wawili.
No comments:
Post a Comment