Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari |
Rais mpya wa Nigeria, Muhammadu Buhari, ameendeleza kile kilichoanzishwa na mtangulizi wake,
Goodluck Jonathan, katika kusaidia sekta ya filamu kwa kuapa kuhakikisha
anasaidia sekta ya filamu nchini humo kutoanguka kutokana na uharamia wa kazi.
Alisema kuwa sekta ya filamu ya Nollywood inafanya
vizuri ila inaweza kuathiriwa na uharamia. Sekta hii ina thamani ya dola
bilioni 5 (sawa na paundi bilioni 3), lakini watengeneza filamu bado wanasota
kutengeneza faida kwa sababu ya uharamia.
Japo ni sinema zinazotengenezwa kwa bajeti
ndogo, visa vya mapenzi, mikasa, usaliti na uchawi ni mambo ambayo yameenea
zaidi barani Afrika. Rais Buhari aliagiza taasisi za ulinzi kuwatambua wale
wote wanaojiingiza kwenye uharamia wa hakimiliki na kuwafikisha kwenye mikono
ya sheria.
Nollywood si sekta pekee inayoathirika na
tatizo hili. Mtayarishaji wa Kannywood – sekta ya filamu za lugha ya Kihausa zinazotengenezwa
katika jiji la kaskazini la Kano – pia analalamika na amemuomba Rais kuingilia
kati.
Rais Buhari amesema atafanya kila awezalo
kuilinda sekta ya burudani ya nchi hiyo. “Wameijenga (watayarishaji wa filamu) sekta
kwa jasho lao,” alisema. “Tuna dhima ya kuhakikisha tunawaunga mkono.”
Wachambuzi wa sekta ya filamu ya Nigeria wanaamini
kwamba Nollywood inatoa sinema 50 kwa wiki. Hata hivyo, nyingi ya sinema hizi zinauzwa
moja kwa moja kwenye DVD na watengenezaji bado wanasota kutengeneza faida.
No comments:
Post a Comment