Watanzania wana mapenzi na sinema au michezo ya TV
kama inavyoonekana kwenye picha hii
NI Jumapili tulivu
inayoambatana na mvua ya rasharasha. Watu kadhaa wamejazana kwenye chumba
kimoja katika nyumba moja wakiangalia filamu ya kusisimua ya Kitanzania. Tukio (scene)
katika filamu hiyo linaanzia pale sebuleni. Ni tukio ambalo linaonekana kuvutia
kiasi; linaikamata dunia ya wapenda sinema na kuwafanya watazamaji hawa waamini
kuwa wanachokiona ni cha kweli.
Katika tukio hilo la kwenye filamu, sebule inaonekana ni ya kuvutia sana . Vitendea kazi vyote
vinavyohitajika kuonesha uhalisia kwenye tukio hilo vimeongezwa. Anaonekana Mama mwenye
nyumba akiwa amekaa kwa raha mustarehe kwenye kochi sebuleni kwake. Amevalia nguo nzuri na
jozi ya ndala yenye rangi sawa na nguo yake. Katika mkono wake, ameshika
gazeti; haonekani kulisoma lakini analitumia tu kwa ajili ya kusukuma muda
uende mbele.
Hili ndilo tukio linaloifungua
filamu ambayo imeshaingia katika soko, na inauzika kama
njugu huku ikipewa ‘promo’ kubwa na magazeti pendwa nchini.
Watayarishaji wa filamu hii
wanatabasamu wakihesabu pesa zao, lakini wakati huohuo waigizaji walioigiza kwenye
filamu hii wanapokea script nyingine kutoka kwa watayarishaji wengine tofauti
ambao wamewaona kuwa wanafaa kupewa majukumu katika sinema zao kufuatia kufanya
vyema kwenye sinema hii.
Matukio katika filamu hii
yanaendelea, mara, kuna tukio kubwa la kisinema linaonekana: kwenye kioo cha televisheni
(screen) anaonekana msanii mmoja mkongwe: na maandishi yaliyoandikwa ‘Miaka 20 baadaye…’
Lakini haichukui muda kwa
watazamaji kugundua kwamba ingawa inasemwa kuwa matukio hayo yanatokea baada ya
miaka ishirini lakini bado mazingira ni yaleyale na hayajabadilika, hakuna
chochote kilichobadilika. Makochi bado ni yaleyale; nyumba bado iko vilevile;
mtu bado ni yuleyule (kwa maana ya umri); mavazi bado ni yaleyale; hata
mwanamke aliyeonekana sebuleni kashika gazeti bado kavaa jozi ileile ya ndala!
Miaka ishirini baadaye! Watazamaji,
kwa hasira, wanaacha kutazama filamu hiyo, mmoja anabadilisha stesheni ambapo
sasa wanaangalia matukio ya wiki katika kituo kimoja cha televisheni.
Hii ndiyo tasnia ya filamu yaTanzania .
Karibuni katika ulimwengu wa sekta ya filamu ya Tanzania . Tasnia yenye nguvu Afrika
Mashariki na katika nchi za maziwa makuu, lakini inayoonekana kukosa mwelekeo
ambao ungeweza kuzifanya filamu zionekane kuwa zimeandaliwa kikamilifu.
Hii ndiyo tasnia ya filamu ya
Kwa miaka mingi, sekta ya
filamu ya Tanzania
imeshuhudia kile kinachoweza kuitwa mapinduzi (japo si kamili), angalau katika
miaka kumi iliyopita. Kutokana na ongezeko la filamu za Kitanzania majumbani
katika miaka ya elfu mbili (baada ya kuzipiga kumbo filamu za Nigeria ), mtayarishaji wa filamu nchini
amelazimika kupitia hatua moja hadi nyingine, ambapo leo, kama
weledi ungezingatiwa nadhani angekuwa katika hatua sita tofauti kuelekea mbele.
Hadi sasa, nje yaTanzania ,
hasa katika nchi zinazotuzunguka za Afrika mashariki na za Maziwa Makuu, bado kazi
zinazotamba ni zile za watu kama Ron Mulvihill
na Marehemu Nganyoma Ng’oge, Profesa Martin Mhando, Profesa Amandina Lihamba na
Geoffrey Mhagama.
Hadi sasa, nje ya
Hata hivyo,
kuna baadhi ya kazi za zama hizi zinazofurahiwa mno, zama ambazo zimeshuhudia
wakiibuka watu mahiri kama Mwl. Kassim Al
Siagi, Amri Bawji na marehemu Hammie Rajabu. Ingawa filamu zao zilitengenezwa
katika mfumo wa analogia (VHS), lakini zimeweza kusisimua hadi leo.
Watayarishaji hawa wa
filamu walijitahidi sana kuhakikisha wakisimulia
hadithi kuhusu Tanzania ,
Afrika na watu wake, japo baadhi zilihusu mapigano. Baada ya hapo, miaka ya
hivi karibuni mwelekeo wa tasnia ya filamu umeonekana kubadilika mno.
Watayarishaji wa filamu
nchini wameonekana kukosa kabisa mafunzo ya msingi ya namna ya kutengeneza kazi
zao katika kiwango kinachokubalika licha ya kazi zao kukubalika kwenye jamii ya
Kitanzania. Kwa mujibu wa tafiti ninazoziamini, watayarishaji wengi wa filamu
nchini ni wabinafsi na wanaowekeza kidogo na kutarajia wavune mara dufu kwa
mara moja.
Ubinafsi wao umekuwa
ukisababisha filamu za Tanzania
zionekane kuwa ni kitu kisichozingatia au kuhitaji taaluma yoyote. Watu
wanalipua kazi watakavyo na wanafanya mambo bila kuzingatia utaalam. Wanafanya
mambo ili mradi wanajua kuwa watauza na kupata pesa, basi.
Ubinafsi wao umekuwa ni sababu kuu ya kuufanya uwanja wa filamu waTanzania kuwa
sehemu inayoongoza kwa kutokuwa na mgawanyo wa majukumu. Si ajabu kuona anayejiita
mkurugenzi wa kampuni ya kutengeneza filamu, ndiye huyo huyo aliyeandika script,
ndiye muongozaji mkuu, ndiye muigizaji mkuu, ndiye atakayehariri na kadhalika.
Ubinafsi wao umekuwa ni sababu kuu ya kuufanya uwanja wa filamu wa
Ni wakati sasa tunahitaji
kufanya mapinduzi ya kweli ya tasnia ya filamu na wala tusisingizie bajeti.
Mapinduzi yatatuweka kwenye ramani nzuri duniani, ili twende sambamba na nchi
za Francophone au Afrika Kusini. Ziko wapi hazina zetu tunazoweza kujivunia
katika ulimwengu wa filamu? Ni lini tutashuhudia filamu zetu au wasanii wetu wakipita
kwenye zuria jekundu katika matamasha ya filamu ya kimataifa au kwenye tuzo
kubwa duniani?
Mwalimu wangu (mentor) aliwahi
kuniambia kuwa ninapofikiria kufanya kazi yoyote ya ubunifu lazima nikumbuke
kuwa binadamu amezungukwa na matabaka makubwa manne katika maisha ili kuufikia
ufanisi wa kazi, matabaka hayo ni: (1) Easy to do; (2) It’s difficult; (3)
impossible; na (4) beyond imagination.
Easy to do: hii ni hatua
ambayo kila mtu huona kuwa jambo alilokusudia kulifanya ni rahisi na linaweza
kufanyika kirahisi tu, ni kama ambavyo watengeneza
filamu wa Kitanzania wamekuwa wakifanya kwa kurahisisha kazi zao bila hata
kujali weledi wakiamini katika matangazo ‘promo’.
It’s difficult: ni hatua
ambayo unaanza kuhisi ugumu fulani kwenye kazi yako na kuanza kuona kuwa ipo
haja ya kujali weledi kwa kuanza kuwatumia baadhi ya wanataaluma. Kuna watu
huanza kukata tamaa katika hatua hii na kuacha kuendeleza vipaji vyao ambavyo
pengine vingewasaidia.
Impossible: ni hatua ambayo
utaona kuwa kitu ulichokusudia hakiwezekani, ni kama ambavyo tunaona kuwa haiwezekani
kabisa siku moja sinema ya Kitanzania kuwa na ubora kama wa sinema za Hollywood . Au haiwezekani
kwa wasanii wa Tanzania siku
moja kuwa kama mastaa wengine wa tasnia
zilizoendelea.
Beyond imagination: mara
nyingi hatua hii inasimama katika ulimwengu wa kufikirika. Ukiishi katika
dhana/hatua hii na kuamini kila mtu atakuona umechanganyikiwa. Hii ni hatua
ambayo unapaswa kufikiria mambo ambayo kwa wengine yataonekana si ya ulimwengu
huu. Kwa mfano; kuwekeza nguvu ukitaraji kutengeneza sinema itakayochukua tuzo
ya Oscar.
Hivi kama mtu mmoja
angesimama mwaka 1964 (wakati Mandela anaingia gerezani) na kusema kuwa siku
moja Mandela atakuwa rais wa Afrika Kusini angeonekanaje, ni mwendawazimu? Kachanganyikiwa?
Na vipi kama mtu mwingine angesimama takribani
miaka kumi tu iliyopita akaiambia dunia kuwa Barack Obama (mtu mweusi) atakuwa
rais wa Marekani angeonekanaje pia? Kapandwa wazimu au anaota ndoto ya mchana?
Lakini leo yote yamewezekana.
Kwa nini tusifikirie kuwa kwa kutumia weledi siku moja sinema ya Tanzania
itachukua tuzo ya Oscarau wasanii wetu siku moja watapita kwenye zuria jekundu
pamoja na kina Will Smith? Kwa sasa huu nao ni wendawazimu, au siyo? Hii ndiyo ‘beyond
imagination’, na kila mmoja anapaswa kuishi katika hatua hii huku akizingatia sana katika ubunifu na
kujali ubora.
Kwa wenzetu Afrika Kusini,
hazina kubwa katika taji la sekta ya filamu ya nchi hiyo ni filamu ya Tsotsi,
kazi iliyofanywa na Gavin Hood, iliyoigiza kuhusu vijana waporaji wa Soweto , karibu na Johannesburg ,
ambayo ilishinda tuzo ya Oscar katika kipengele cha filamu za lugha ya kigeni
mwaka 2006.
Si hiyo tu, wana filamu
nyingine iliyowahi kuteuliwa kushiriki tuzo ya Oscar ya Yesterday, iliyochezwa
na Leleti Khumalo, na ilishawahi kushinda katika tuzo mbalimbali za kimataifa,
na U Carmen E Khayalitsha, iliyopigwa katika lugha ya Xhosa ambayo ilishinda
tuzo ya Golden Bear mwaka 2005 katika Tamasha la Filamu la Kimataifa la Berlin . Filamu hizi
zimetia chachu kwa watengenezaji wa filamu wa Afrika Kusini kuwa wabunifu na
wenye kujali ubora (wanaoishi katika beyond imagination).
Faida za ukuaji wa sekta ya
filamu ziko wazi, hasa linapokuja suala la kuingiza fedha za kigeni, ushiriki
katika uzalishaji na matokeo ya makampuni ya kimataifa katika uwekezaji wa moja
kwa moja wa mamilioni ya shilingi katika uchumi.
Tunahitaji kuona siku moja
mastaa wa filamu nchini wakiishi maisha mazuri tofauti na ilivyo sasa. Kwa sasa
fani hii imekuwa ikiingiza fedha nyingi tofauti na ilivyokuwa awali, lakini maslahi
hayo huishia kwa wasambazaji na watayarishaji/wasanii wachache ambao
hawashikiki.
Wasanii kwa sasa wamejijengea
majina kwenye jamii ya wapenzi wa filamu kufikia kiwango ambacho bila wao kazi
hazinunuliki madukani na baadhi ya maprodyuza wameeleza kuwa wengine hata
kutokea sura zao ni biashara tosha hata kama
wameigiza upuuzi. Lakini nini hatima yao ?
Kuuza sura bila mafanikio? Mimi nadhani tuanze mabadiliko sasa na tuachane na
blah blah.
Naomba kuwasilisha.
No comments:
Post a Comment