Filamu hiyo ya Chungu iliibuka kidedea katika tuzo hizo
baada ya kufanikiwa kuwa filamu bora huku pia ikitoa mwigizaji bora wa Tanzania , Richard Mshanga, maarufu kama Masinde ambaye katika filamu hiyo alitumia jina la
She Mdoe.
Filamu ya Chungu imezungumzia mazingira ya kijamii hususan
masuala ya kishirikina ambapo She Mdoe alikuwa akituhumiwa kama
muuaji wa vikongwe kwa tuhuma za kichawi.
Chungu imeandaliwa katika Mkoa wa Tanga eneo la Bumbuli
ikiandaliwa na Kampuni ya Shule & Co. na muandaaji wa filamu hiyo ni Dk. Vicensia
Shule ambaye ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Idara ya Sanaa na Maonesho,
na imeongozwa na Kimela Bila.
Kwa kauli yake, Vicensia Shule anasema kuwa katika
kuitengeneza filamu hii alikuwa akifanya utafiti, na hii
ni filamu yake ya pili ya utafiti katika masuala ya filamu nchini, aliamua kuingia
katika fani ya uandaaji wa filamu ili kufahamu changamoto mbalimbali zinazoikabiri
tasnia ya filamu.
Pia aliongeza kuwa: Filamu yake ya kwanza ya utafiti
ilijikita katika upande wa kutambua tabia za waandaaji, waongozaji wa filamu na
tabia za wasanii nchini. Hususan katika mazingira yao
ya kazi na maisha yao
kwa ujumla na filamu hii ya Chungu ikawa
sehemu ya pili ya utafuti wake huku mara hii akihitaji kujua
mazingira ya wasambazaji na kipato kinachotokana na kazi hiyo pamoja na kipato
kinakwenda kwa wasanii wenyewe.
Mhadhiri huyo alisema kwamba asingeweza kuandika ripoti
nzuri kuhusu tasnia ya filamu nchini bila kuingia katika kazi hiyo kwani kwa
kufanya hivyo imemsaidia kujua maisha anayoishi muandaaji wa filamu pamoja na
kipato chake, pia amepata kujua maisha ya msanii na muongozaji pamoja na vipato
vyao.
na hakuishia hapo, pia amefanikiwa kujifunza maisha anayoishi msambazaji na kwamba baada ya kujua changamoto hizo zote sasa anajipanga kutengeneza filamu itayoweza kuleta mabadiliko katika tasnia ya filamu nchini huku pia akijiandaa kuandika ripoti itakayoweza kutoa njia za kutatua changamoto hizo.
No comments:
Post a Comment