Meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania, Barbara
Kambogi, akizungumza katika semina fupi ya wadau wa Tasnia ya Filamu nchini
pamoja na waandishi wa habari
Mashindano ya Tuzo za Filamu Afrika (AMVCA) yatakayofanyika
jijini Lagos, Nigeria Machi 9 mwakani na kushirikisha wasanii na watengenezaji
wa filamu barani Afrika yalizinduliwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam
katika hafla iliyoshirikisha makundi mengi ya filamu nchini.
Hafla hii imekuja kufuatia matukio mengine mawili
yaliyofanyika mjini Lagos na Nairobi ,
ambapo AfricaMagic na Multichoice Africa walitangaza mpango wao mpya
unaojulikana kama ‘Tuzo za Chaguo la
Watazamaji wa AfricaMagic’.
Tangazohilo la
kusisimua lilitolewa wakati wa sehemu ya kisa muhimu cha onesho lililofanyika
usiku katika gazeti maarufu la AfricaMagic, linalooneshwa kwenye luninga kwa
watazamaji wa DStv katika nchi 47 za Afrika.
Ikiwa imetengenezwa kuadhimisha kipaji cha Afrika katika filamu na televisheni, mbele na nyuma ya kamera, tuzo hizo zitakuwa na vipengele kadhaa muhimu, ambavyo watazamaji watachagua washindi wao moja kwa moja pamoja na vipengele kadhaa vilivyopangwa kitaalamu.
Tuzo hizo zitahusu filamu zilizotengenezwa kwa lugha za Kiingereza, Kiswahili, Kihausa na Kiyoruba zilizotungwa kati ya Mei Mosi, 2011 na Aprili 30, 2012. Aidha jumla ya vipengele 26 vitashindaniwa katika mashindano hayo na kwamba washindi katika kila kipengele watapatikana kwa kupigiwa kura na watazamaji wa filamu barani Afrika sambamba na maoni ya majaji walioandaliwa kwa ajili ya tuzo hizo.
Tangazo

Vipeengele vitakavyoshindaniwa ni pamoja na ‘Msanii Bora wa
Kike’, ‘Msanii Bora wa Kiume’, ‘Filamu Bora ya Kiswahili’, ‘Filamu Bora ya
Mwaka 2012’, ‘Mwandishi Bora wa Filamu’, ‘Mchekeshaji Bora’, ‘Msambazaji Bora
wa Filamu’, ‘Muongozaji Bora wa Filamu’.
Mwisho wa wasanii kutuma kazi zao ni Oktoba 31. Wasanii wa Tanzania wana nafasi kubwa ya kuchukua tuzo
nyingi ikizingatiwa kuwa katika kituo cha AfricaMagic asilimia 80 ya filamu
zinazorushwa ni za Tanzania .
Hata hivyo washindi wa vipengele vyote vinavyoshindaniwa
watapata tuzo maalum za heshima na kwamba, hapatakuwa na zawadi za fedha.
No comments:
Post a Comment