Sajuki, enzi za uhai wake
Watu wengi wamepokea taarifa ya kifo cha Msanii maarufu wa
filamu nchini Tanzania Sadiki Juma Kilowoko au Sajuki kama
ambavyo anajulikana na wengi aliyefariki dunia alfajiri ya kuamkia leo katika
hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salam alikokuwa akitibiwa.
Sajuki anajulikana na wengi kwa sinema zake za kashkash
alikuwa akiugua maradhi ya muda mrefu mpaka kufikia hatua ya kupelekwa India
kwa matibabu zaidi.
Inaeleweka kwamba msanii huyo alikuwa anaugua na
maradhi yaliyosababisha uvimbe ndani ya tumbo lake
lakini kwa msaada wasamaria wema
waliweza kumchangia na kumfanya apate matibabu nchini India ambapo hali yake iliendelea kuimarika na
kuwa nzuri kwa afya yake na kurudi Nchini Tanzania .
Sajuki ameacha mjane ambaye pia ni msanii aitwaye Wastara Juma
ambaye ni mlemavu wa mguu mmoja ambao ulisababishwa kwa kupata ajali mwaka 2008,
siku chache kabla ya ndoa yao .
Hata hivyo Sajuki aliamua kumuoa hivyo hivyo kwani alikuwa ameshapeleka posa
kwa kina Wastara.
Tukiohilo liligusa hisia za watu wengi na
kumchukulia Sajuki kama shujaa na mwanaume
mwenye mapenzi ya kweli kwa kitendo hicho alichokifanya.
Mwaka 2011 haukuwa mzuri kwa Sajuki kwani ndio mwaka ambao maradhi yaliyomsumbua muda mrefu yalipamba moto. Inajulikana kuwa Sajuki aliumwa na kufikia kipindi cha kudhoofu mwili wake kitu kilichosababisha wasanii wenzake na watu wengine waanzishe mchango wa kumchangia Sajuki.
Wasanii, wanasiasa, wananchi walifanikisha zoezihilo
na kumfanya aweze kwenda India
kwa matibabu zaidi. Alirudi na kuonekana kapata nafuu kidogo jambo ambalo
lilileta nyuso za furaha na amani miongoni mwa Watanzania.
Hata hivyo alikuwa hajapona sawa sawa na alikuwa anajiandaa kurudi tenaIndia kwa
matibabu zaidi, na hii alikiri kwenye kipindi cha 'Mkasi' kinachoendeshwa na
kituo cha televisheni cha EATV.
Sajuki ambaye ni Mngoni ameshacheza maigizo na filamu na wasanii wengi karibia wote wenye majina hapaTanzania .
Sajuki kwa kusaidiana na mkewe walifungua kampuni ya productions kwa
ajili ya filamu (movies) za hapa hapa nchini.
Tukio
Mwaka 2011 haukuwa mzuri kwa Sajuki kwani ndio mwaka ambao maradhi yaliyomsumbua muda mrefu yalipamba moto. Inajulikana kuwa Sajuki aliumwa na kufikia kipindi cha kudhoofu mwili wake kitu kilichosababisha wasanii wenzake na watu wengine waanzishe mchango wa kumchangia Sajuki.
Wasanii, wanasiasa, wananchi walifanikisha zoezi
Hata hivyo alikuwa hajapona sawa sawa na alikuwa anajiandaa kurudi tena
Sajuki ambaye ni Mngoni ameshacheza maigizo na filamu na wasanii wengi karibia wote wenye majina hapa
No comments:
Post a Comment