Dk. Vicensia Shule, akitoa dukuduku lake kuhusiana
na changamoto za urasimishaji
Mkutano huo ulikuwa na ajenda zifuatazo:
i.
Kufungua mkutano
ii.
Kutoa muhtasari wa madhumuni ya serikali na hatua
zilizofikiwa hadi sasa
iii.
Kuelezea hatua za upatikanaji wa stempu za kodi
iv.
Kupata taarifa ya hali halisi ya upatikanaji wa mashine
za kubandika stempu
v.
Kuzungumzia mikataba kati ya wafanyabiashara na wasanii
vii.
Kupata maoni ya wasambazaji na kujua tofauti kati ya
bidhaa za filamu na muziki
viii.
Kufanya majumuisho
ix.
Kufunga kmkutano.
Baadhi ya yaliyojadiliwa na wadau:
- Projection & stock -Wasambazaji walionesha wasiwasi
juu ya mfumo wa kununua stika ilihali kuwa haijulikani idadi gani ya kazi
utakazouza. Walipendekeza TRA iwarudishie rejesho la pesa kwa kazi ambazo
hazikuuzika baada ya kubandikwa stampu.
- Wadau wakiwemo wazalishaji na wasanii walihoji uasili na
wakati gani wa kuharibika kwa kazi za sanaa kwenye soko ili kuhalalisha madai
ya wazalishaji, kinyume chake waliomba ufafanuzi kwa TRA inafanyaje kwa kazi
zinazoonekana haziuzi leo lakini zitauzwa hata baada ya miaka kumi (ambapo TRA
haikuweza kutoa ufafanuzi wa kueleweka juu ya hilo)
- CONFUSSION -Wadau walionekana kutoridhishwa na baadhi ya
majibu yaliokuwa yakitolewa bila mchanganuo wa kueleweka Likiwemo la
Mfanyabiashara kupewa ruhusa ya kujiunga na mfumo wa VAT mara baada ya kufikia
kiwango fulani cha mauzo yake ya mwaka pasi na kuainisha faida au hasara
zilizomo ndani yake.
- TRA kupokea moja kwa moja ushauri wa kutumia njia ya
kienyeji “manually” kubandika stamp kutoka kwa Msambazaji mkubwa na kuiweka
kando njia ya kutumia mashine kwa kisingizio cha kukuza ajira kwa watu
wanaotumiwa kubandika hizo stika/stampu au uharaka wa kazi imeleta sura
mpingano kwa wadau na wasanii juu ya kuchomoza kwa mianya ya piracy. Wameiomba
TRA ifanye utafiti wa kutosha na isikurupuke tu.
- ULINZI - Kwa mujibu wa TRA stamp zitakazotolewa zitatolewa
kwa title (yaani kwa kila kazi ) na pia zitakuwa na Code namba ambazo
zitasaidia licha ya uzuiaji wa wizi pia kujua jumla ya mauzo kwa kazi husika.
Kazi ya ku-monitor hili itafanywa na TRA ikishirikiana na kamati zake (Bodi ya
Filamu, Cosota na Basata) kamati ambazo baadhi yake zimeonekana kuwa na
mapungufu mengi ya utawala na utendaji. (Vipi tunarasimisha sekta ilihali bado
kamati zinatotegemewa na mchakato mzima zina mapungufu?)
- Pia tumeambiwa kwamba ukaguzi wa kujua mauzo ya stamp
yameendaje, mfumo wake utakuwa ni kukagua stamp ngapi ya zile zilizotolewa na
TRA zimebakia, jambo hili bado linatupa mashaka ya mfumo huo kama
utakuwa na ulinzi imara wa kazi hizo.
Hata pendekezo la kutumia bar code kwa atakayependa kutumia
mfumo huo hautoi ulinzi wa mfanyabiashara kuifuatilia kiurahisi bidhaa yake na
kuikagua kama halali ama piracy.
- TRA imeshindwa kufafanua itawiainishaje juu ya mfumo wa
biashara unaoendana na maendeleo ya Techologia (Teknohama) na mfumo wa
ubandikaji stamp wakati hali halisi inaonekana kuwa inatia nguvu kubwa katika
hard copy ambayo digitally inafutika polepole.
- Wasambazaji wameeleza kuwa sheria haiwabani wanaofanya kazi za Library, kwenye mabasi na mahoteli ambao wanasababisha mapato kuwa madogo hivyo watashindwa kununua stamp.
- Wasambazaji wameeleza kuwa sheria haiwabani wanaofanya kazi za Library, kwenye mabasi na mahoteli ambao wanasababisha mapato kuwa madogo hivyo watashindwa kununua stamp.
- Wadau wameiomba serikali kupitia TRA kuongeza kodi au bei
ya stamp za kazi zinazotoka nje za sanaa ikiwemo za 10 In 1 ili kumarisha soko
la ndani.
- TRA imekiri kuwa kuna ugumu wa kuzui kazi za ndani ambazo
zinauzwa kiharamia nje ya mipaka yetu kutokana na nchi kuwa na mifumo ya Tax
force inayotofautiana. (Hivyo imelichukua hilo kama changamoto)
- Wadau wameiomba TRA iangalie sheria ya Cosota ya mhalifu
wa kazi za sanaa kulipa faini isiyoendana na ukubwa wa kosa. Kinyume chake
wasanii watashindwa kuamini kwamba mfumo huu ni kwa ajili ya kusaidia kulinda
kazi zao.
- TRA imeonekana ina wasiwasi juu yakama
itaweka sheria ambayo itawabana wasambazaji ambao ndio pia wana capital kubwa
kulinganisha na wasanii, Wasambazaji watabadilisha biashara hivyo mfumo hautoi
function. Kimsingi TRA wanatakiwa wafanye tafiti ambazo zitasaidia kuja na
mfumo bora utakaosaidia kuongeza wazalishaji na wasambazaji wenye ubora kwenye
tasnia hizi mbili.
- Wadau wameiomba TRA isaidie kuweka mifumo ambayo wasanii, wazalishaji n.k waweze kusaidiwa kuwa wafanyabishara wasambazaji wa kazi zao kwa kuwapa mikopo na mifano yake. Hiyo pia itaongeza idadi ya walipa kodi.
MIKATABA:
- TRA imeonekana ina wasiwasi juu ya
- Wadau wameiomba TRA isaidie kuweka mifumo ambayo wasanii, wazalishaji n.k waweze kusaidiwa kuwa wafanyabishara wasambazaji wa kazi zao kwa kuwapa mikopo na mifano yake. Hiyo pia itaongeza idadi ya walipa kodi.
MIKATABA:
- Ni suala lililoelezewakuwa na mapungufu makubwa. Zifuatazo
ni miongoni mwa sababu zilizoelezwa na wadau kuwa ni matatizo ya mikataba:
- Kutoshirikisaha wanasheria, kutotaka kufanya tafiti au
hata kutotaka kutumia tafiti, ukosefu wa elimu ya kugundua/kutambua lugha za
kitaalamu ama kisheria.
Hivyo walipendekeza yafuatayo:
- Mikataba iwe ya Kiswahili kinachoeleweka. Wakati wa usainishaji wa mikataba kuwepo na chombo kimojawapo kama Basata au Bodi kusimamia haki za msingi, kila pande iwe na mwanasheria, Taasisi za kisanaa kama TAFF n.k wanatakiwa kuwapa elimu watu wake kuhusu faida au hasara inayopatikana na uuzaji wa hakimiliki na hakishiriki na pia kuwa na azimio la pamoja kimsimamo kwa wote juu ya kiwango cha kazi kabla ya kuingia mikataba
VALUE CHAIN:
Wachangiaji wameweza kugawanya mfumo wa mnyororo wa dhama
(Value Chain) Tanzania katika sehemu mbili:
- Mfumo wa nadharia na Mfumo wa Uhalisia (mazoea)
- Mfumo wa nadharia na Mfumo wa Uhalisia (mazoea)
- Nadharia ni mfumo unaotumika katika nchi nyingi kuanzia kwa mwandishi mpaka kwa msambazaji na mnunuzi wakati Mfumo wa Uhalisia ni huu ambao unaotumika Tanzania pekee wa Msambazaji kulazimisha,kupendekeza filamu iwe vipi. Wadau wamedai kuwa mfumo huu ndio umepelekea uvunjwaji wa maadili na kuharibu dhima nzima ya uandishi kulingana na mafundisho badala yake inakuwa ni uandishi kulingana na wasambazaji wanataka nini au wanamtaka nani acheze
MAJUMUISHO:
- TRA wamependekeza licha ya kikao cha leo kuitisha semina nyingine za kutoa elimu juu ya Sheria na mikataba.
- Wadau wameshauri TRA itanue upeo wa kutoa elimu nchi nzima
ikiwezekana iwe na kipindi cha Tv.
- Pia wameshauri kuwa wafungue kundi katika mitandao ya jamii ili wadau waweze kujadiliana kupitia online hivyo watakuwa wamefikisha maoni ambayo yanaweza yakawa na tija kwao na tasnia nzima.
Kufungwa Kikao. Kikao kilifungwa rasmi huku TRA wakiahidi watatoa Taarifa kwa wadau katika kikao kifuatacho.
No comments:
Post a Comment