Moja ya kazi nzuri zilizotengenezwa Afrika Kusini
SEKTA ya filamu ya Afrika
Kusini ni mahiri, inayokua na kuzidisha ushindani katika anga za kimataifa. Watengenezaji
wa filamu wa ndani na wa nje wanatumia fursa mbalimbali zilizopo, maeneo ya
kipekee - na gharama nafuu za uzalishaji na kiwango kizuri cha pesa ya Afrika
Kusini dhidi ya dola ya Kimarekani, ambacho hufanya kuwepo unafuu wa hadi
asilimia 40 katika kutengeneza filamu Afrika Kusini kuliko Ulaya au Marekani na
unafuu wa hadi asilimia 20 zaidi kuliko Australia.
Hazina katika taji la sekta
ya filamu ni Tsotsi, kazi ya Gavin Hood iliyoigiza kuhusu vijana waporaji wa Soweto , karibu na Johannesburg ,
ambayo imeshinda tuzo ya Academy katika kipengele cha filamu bora za lugha ya
kigeni mwaka 2006.
Filamu nyingine iliyoteuliwa
kushiriki kwenye tuzo ya Oscar ni Yesterday iliyochezwa na Leleti Khumalo, na
ilishinda katika tuzo mbalimbali za kimataifa. Filamu hii inaelezea kisa cha mama
mwenye VVU anayepambana, na U Carmen E Khayalitsha, iliyopigwa katika lugha ya Xhosa
ambayo ilishinda tuzo ya Golden Bear mwaka 2005 katika Tamasha la Filamu la Berlin,
zimetia chachu ya watengenezaji wa filamu nchini Afrika Kusini kuwa wabunifu na
wenye kujali ubora.
Kutokana na sifa hii, sinema
nyingi za bajeti kubwa na zenye mafanikio makubwa za kimataifa zimekuwa zikipigiwa
nchini humo, ikiwa ni pamoja na Blood Diamond iliyomshirikisha Leonardo
DiCaprio na Lord of War, iliyomshirikisha Nicholas Cage akicheza kama muuza
silaha duniani, Lord of War imesaidia kutangaza maeneo tajiri nchini Afrika
Kusini – huku eneo la Cape Town likionekana kama maeneo tofauti 57 yaliyofanywa
kuonekana kama meneo katika Mashariki ya Kati, Afghanistan, Bolivia, Sierra
Leone na kwingineko.
Fursa nyingi, pamoja na
waandaaji wa sinema, biashara na uzalishaji mwingine ni vivutio vilivyofanya watengenezaji
wa Afrika Kusini wenye ujuzi wa filamu na watendaji wengine, vifaa bora vya
kiufundi na miundombinu mizuri - na hali nzuri ya hewa.
Serikali ya Afrika Kusini
imetambua kuwa sekta ya filamu ni sekta yenye nguvu na inayochangia kwa kiwango
kikubwa ukuaji wa uchumi. Ingawa mchango wa Afrika Kusini kwa pato kimataifa unasimama
katika asilimia 0.4 tu, sekta ya filamu kwa ndani ya Afrika Kusini inazidi
kupata nguvu wakati wote.
Mwaka 1995, wakati nchi hiyo
ilipoanza kutumika kama eneo muhimu kwa ajili
ya uzalishaji wa filamu na televisheni, sekta hiyo ilitoa ajira nchini kote kwa
watu 4 000. Imepanda hadi kufikia watu wapatao 30,000, pamoja na ajira zaidi -
na mapato – vikitengenezwa katika filamu - ikihusisha usafiri, malazi na chakula.
Kwa mujibu wa Idara ya
Biashara na Viwanda, sekta ya burudani nchini Afrika Kusini ina thamani ya
karibu Randi bilioni 7.4, huku filamu na televisheni zikichangia zaidi ya Randi
bilioni 5.8 katika shughuli za kiuchumi kila mwaka. Na kulingana na matokeo ya utafiti
wa tathmini ya kiuchumi ya hivi karibuni uliosimamiwa na Tume ya Filamu ya Cape , sekta hiyo ina mapato ya moja kwa moja kila mwaka
ya zaidi ya Randi bilioni 2.65 na huchangia mapato ya moja kwa moja kila mwaka
ya zaidi ya Randi bilioni 3.5 ya pato la taifa la nchi hiyo (GDP).
Faida za ukuaji haraka wa sekta
ya filamu ziko wazi, hasa linapokuja suala la kuingiza fedha za kigeni. Ushiriki
katika uzalishaji na matokeo ya makampuni ya kimataifa katika uwekezaji wa moja
kwa moja wa mamilioni ya randi katika uchumi.
Afrika Kusini imetiliana
saini mikataba ya ushirikiano katika uzalishaji filamu wa pamoja na nchi nne: Canada , Italia,
Ujerumani na Uingereza. Hii inamaanisha kwamba ushirikiano katika uzalishaji
filamu wowote rasmi unachukuliwa kama
uzalishaji wa kitaifa kwa kila nchi mwenza iliyohusika katika uzalishaji, hufanya
hivyo kwa faida au mipango ya kwa msaada wa kila nchi inayohusika. Afrika
Kusini pia ina mkataba wa makubaliano kuhusiana na filamu na nchi ya India .
Afrika Kusini ina historia
ya muda mrefu katika utengenezaji wa filamu, ilianza kupiga picha za sinema
wakati wa Vita Kuu ya Waafrika-Makaburu katika karne iliyopita miaka ya 1910. Filamu
ya kwanza ndefu ya Afrika Kusini, The Kimberly Diamond Robbery, ilitengenezwa
mwaka 1910.
Serikali ya Afrika Kusini
imekuwa ikisisitiza umuhimu wa filamu katika kujenga urithi wa nchi hiyo kwa
kuwasimulia watu hadithi zao wenyewe, na imejiweka katika “kuwezesha udhibiti”
kwa kuhimiza uzalishaji wa bidhaa za ndani.
Vyombo vya utangazaji vya
Afrika Kusini vimekusudia kufikia lengo la kutoa kipaumbele kwa kazi huru za
ndani, ambazo zimesababisha kuongezeka kwa mahitaji ya vipindi vya ndani. Zaidi
ya tamthilia saba zinazorushwa kila siku Afrika Kusini zinazalishwa nchini
Afrika Kusini.
"Ni maadili muhimu ya
taifa ya kujenga majukwaa ya Waafrika Kusini wa kawaida kuwa na uwezo wa kubeba
ushawishi katika maelezo ya picha zao wenyewe," anasema Eddie Mbalo,
mtendaji mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Filamu na Video (NFVF). "Kwa njia
hii, kama sekta, tunaweza kuchangia kuendeleza
maadili yetu ya kidemokrasia na kuleta mafanikio."
Vyombo vya utangazaji vya
Afrika Kusini vimeanza kuchunguza fursa ya kusambaza kazi za ndani katika nchi
nyingine za Afrika kwa njia ya mauzo ya moja kwa moja na aina ya biashara za
mabadilishano, ambapo mabara hubadilishana vipindi kwa ajili ya matangazo. Hii
inatarajiwa kuongezeka kwa mahitaji ya kazi zinazozalishwa ndani ya nchi.
Watengenezaji filamu wa kimataifa
na wazalishaji pia wanalengwa kwa Randi milioni 430, studio za filamu kama za Hollywood
zinajengwa nje ya jiji la Cape Town .
Ushirikiano kati ya umma na watu binafsi, jukwaa la mafunzo kuhusu sauti – ili kukidhi
mahitaji ya watengenezaji filamu wa ndani na wa kimataifa - lilitarajiwa
kukamilika 2010.
Wanahisa katika mradi wa
Studio za Filamu za Cape Town - zamani walijulikana
kama Dreamworld - ni pamoja na Videovision, Sabido Investments, the Rico Trust,
the Helderberg African Chamber of Commerce, na Taasisi ya biashara na uwekezaji
ya Western Cape .
Serikali, kupitia Taasisi
ya Taifa ya Filamu na Video (NFVF), Shirika la Maendeleo ya Viwanda na Idara ya
Biashara na Viwanda, ni mwekezaji mkuu katika sekta ya filamu.
Taasisi ya Taifa ya Filamu
na Video husaidia katika upatikanaji wa fedha katika tasnia, kupromoti
maendeleo ya watazamaji wa filamu na televisheni wa Afrika Kusini, kuendeleza
vipaji na ujuzi katika nchi - kwa msisitizo maalum kwa makundi maalum - na kuwasaidia
watengeneza filamu kuwakilisha na kuuza kazi zao kimataifa.
NFVF hutoa fedha kwa ajili
ya uzalishaji wa filamu na makala (documentaries) kwa njia ya mikopo au ruzuku.
Husaidia makampuni ya uzalishaji yanayomilikiwa na Waafrika Kusini, na hutoa kipaumbele
kwa miradi au mashirika yanayoweka umuhimu wa kitaifa na mapendekezo ambayo
yanasisitiza kazi za ndani na ambayo yana uwezeshaji au mafunzo.
Pia inagharimia fedha za
elimu na mafunzo kwa njia ya masomo mbalimbali; kutoa tuzo za maendeleo; na misaada
ya maombi ya fedha kwa ajili ya uuzaji na usambazaji, inaruhusu wazalishaji filamu
wa kujitegemea na wasambazaji upatikanaji wa maeneo ya kuoneshea filamu na
uzinduzi wa filamu. Mnamo Machi 2007, NFVF ilitoa kiasi cha Randi milioni 26 katika
ruzuku.
Taasisi ya maendeleo ya
fedha inayomilikiwa na serikali, Shirika la Maendeleo ya Viwanda (IDC)
imekusudia kujenga sekta endelevu ya filamu ambayo ujuzi utasambaa kwa watu
kutoka makundi yaliyokuwa chini ya ubaguzi wa rangi na "kazi za ndani"
za filamu zinatengenezwa na kuangaliwa na Waafrika Kusini.
Kituo cha utoaji fedha cha Mkakati
wa Biashara ya Filamu na Habari cha IDC, mradi wa utangazaji na uhariri. Msaada
ya fedha kwa kawaida hutolewa katika mfumo wa mkopo. Ushiriki wake wa chini ni
Randi million 1 na si zaidi ya asilimia 49 ya mradi. Mnamo Juni, 2008, IDC
imewekeza zaidi ya Randi milioni 500 na kufadhili filamu zaidi ya 30 nchini
humo.
Idara ya Biashara na
Viwanda (DTI) inatoa motisha maalum katika sekta ili kuhamasisha kazi za ndani
pamoja na kuvutia uzalishaji wa kimataifa. DTI imetangaza marekebisho ya motisha
za uzalishaji filamu na vipindi vya televisheni mnamo Machi 2008, ikiondoa
kizingiti na kufungua mlango kwa ajili ya filamu za bajeti ndogo kutoka kwa
watengeneza filamu wanaoibukia.
Motisha ya fedha inatolewa katika
Uzalishaji Filamu na vipindi vya Televisheni wa Afrika Kusini na Ushirikiano ili
kusaidia uzalishaji wa bajeti angalau Randi milioni 2.5 (takriban dola 310,000).
Motisha inatolewa ikiwa na punguzo la asilimia 35 ya gharama kwa filamu na kipindi
cha televisheni kwa Randi milioni 6 (dola 745,000) zilizotumika na asilimia 25
kwa salio la matumizi ya uzalishaji.
Motisha katika Maeneo ya
uchukuaji picha za Filamu na Televisheni inalenga kuvutia filamu za nje za bajeti
kubwa na vipindi vya televisheni. Inatoa punguzo la asilimia 15 kwa wazalishaji
wa kigeni na Waafrika Kusini waliotumia angalau Randi milioni 12 (karibu dola
za Marekani milioni 1.5). Miradi yote, imewekwa kufanya kazi hadi 2014.
mipango mingine ya DTI imelenga
kuendeleza sekta pamoja na: Uwezo wa kuendeleza makampuni ya uzalishaji
yanayoibuka; Maendeleo ya waandishi na wahariri kwa njia ya Mpango wa Maendeleo
ya Biashara wa DTI; Uanzishwaji wa mipango mitano ya majaribio katika maeneo
mbalimbali ili kushughulikia miundombinu ya usambazaji, bidhaa za ndani na
kuongeza watazamaji.
Taasisi tatu za kikanda -
Tume ya Filamu ya Cape, Tume ya Filamu ya Gauteng
na Ofisi ya Filamu ya Durban - zimeanzishwa kuisaidia
kuitangaza miji yao kama
maeneo muhimu na kujenga mazingira mazuri kwa watengeneza filamu.
Mipango ya msaada ya Tume
ya Filamu ya Gauteng ,
kwa mfano, ni pamoja na kusaidia ufadhili na usimamizi wa fedha, na mazungumzo
ya ushirikiano ya uzalishaj na miradi ya ushirikiano na utangazaji.
Huduma ya Mapato ya Afrika
Kusini, katika Sehemu ya 24 F ya Sheria ya Kodi ya Mapato, hutoa ruzuku ya
punguzo la gharama za uzalishaji wa filamu kwa mmiliki wa filamu. Haiunganishi
makato yoyote katika gharama za uzalishaji, au posho yoyote inayohusiana na
hicho, chini ya masharti yoyote ya Sheria ya Kodi ya Mapato, hutoa posho ya
filamu badala yake. Sehemu ya 24 F pia inaeleza kwamba mmiliki wa filamu anaweza
kukata posho ya filamu kutoka kwenye mapato yake.
No comments:
Post a Comment