May 11, 2012

Bila sera nzuri ya filamu hatufiki kokote


Dk. Fenella Mukangara, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

NANI anaweza kunihakikishia kuwa tuna sera ya filamu? Je, sera ya filamu nchini ni ipi? Kama kweli tunaamini kuwa tasnia ya filamu ni moja ya sekta zenye nguvu na yenye kuchangia kwa kiwango kikubwa katika ajira kwa vijana, kwa nini hatuna sera inayotuongoza? Tutaendelea kuongozwa na matamko ya viongozi hadi lini? Ieleweke matamko si sheria, ndiyo maana kila kiongozi anayeingia anakuwa na matamko yake ambayo atakayefuata baada yake halazimiki kuyafuata.

Hivi hatuoni kama huu ni muda muafaka wa kuwa na sera ya filamu itakayotuongoza katika kutenda kazi zetu? Mbona kuna sera ya utamaduni japo hata huo utamaduni wenyewe unapuuzwa? Lakini ipo! Vipi kuhusu filamu?
Sera ya utamaduni ilizinduliwa Agosti 23, 1997 mjini Dodoma, hii ikiwa ni hatua ya pili baada ya ile ya kwanza ya kuundwa kwa Wizara ya Utamaduni wa Taifa na Vijana mwaka 1962.

Ieleweke kuwa nchi yoyote iliyoendelea kwenye tasnia ya filamu ina sera madhubuti, sera inayoangalia pia masoko na ubora wa elimu ya filamu inayopatikana au wanayoitaka. Je, hapa kwetu kuna mwelekeo wa wazi na ushawishi wa kiwango gani katika mafunzo? Kwa kuwa sijawahi kuiona sera yetu ya filamu, naamini tunapaswa kuwa na sera ambayo pia itatusaidia katika utafiti, mafunzo na maendeleo.

Filamu zimeibuka kuanzia karne ya ishirini na baadaye kuwa kishawishi kikubwa na mawasiliano ghali katika karne ya ishirini na moja. Hakuna aina nyingine ya sanaa ambayo imesambaa kwa ufanisi na kuonekana kuvuka mipaka ya kiutamaduni katika mataifa mengi.

Katika karne hii, teknolojia ya televisheni na maonesho mbalimbali ya wajasiriamali vimeitangaza sana tasnia ya filamu kwa watu wote; watazamaji wa mijini na vijijini katika nchi nyingi zinazoendelea. Hata hivyo, filamu nyingi zinazosambazwa kimataifa na kupenya soko la nchi nyingi ni zile zinazozalishwa nchini Marekani na baadhi ya nchi za  Ulaya. Ukweli huu, pamoja na kutambua nguvu ya filamu “inayoyumbisha mioyo na akili za watu” unaamsha wasiwasi kwa walio wengi.

Tangu miaka ya 1960, mjadala kuhusu filamu kutumika kama chombo cha “ubeberu wa kitamaduni” na nchi za Magharibi umekuwa mkubwa, na imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kinadharia.

Filamu pia zimeweza kutumika kama njia muhimu ya uchumi, hali iliyosababisha filamu kugunduliwa Ulaya na Amerika ya Kaskazini. Marekani ilipata udhibiti wa haraka wa soko la filamu mara picha za sauti zilipoanza; ni nchi nyingine chache sana wakati huo ziliweza kumudu kuwa na vifaa bora vya uzalishaji wao kwa haraka kama ilivyokuwa Marekani.

Filamu huweza kutoa ujumbe tofauti kwa kila mtazamaji na huweza kushawishi na kutoa majibu ya kipekee kwa kila mtu binafsi, hivyo, wakosoaji wachache wamejaribu kupima matokeo ya athari zinazosababishwa na filamu zinazoweza kupatikana ama kwa mtu binafsi au watazamaji wote.

Tafiti chache zilizofanywa zimeonesha kuwepo ushawishi mkubwa wa filamu katika majukumu ya kijamii na mahusiano katika jamii ya nchi za Dunia ya Tatu, na hata umakini kidogo umetumiwa kama kigezo katika matumizi ya filamu kama njia ya kuchangia au kubadilisha nguvu ya miundo iliyopo ndani ya mataifa haya au kati ya vikundi vya kikabila au makundi ya kisiasa.

Kumekuwepo mjadala kama hali ya sasa katika soko la filamu/video linaweza kujulikana kama sekta rasmi ambapo mitaji, mitambo na rasilimali zipo kila mahali.

Kwa nchi ya Nigeria, moja ya maendeleo ya kutia moyo sana ni uwepo wa sera ya filamu kwa nchi hiyo. Historia ya sera hiyo inaanzia mwaka 1991 wakati Shirika la Filamu la Nigeria (NFC) lilipoandaa jopo kuangalia kanuni zilizokuwepo kwa lengo la kuoanisha na kuhuisha kiini cha sera ya filamu.

Sera ya filamu bahati nzuri ndiyo hati nzuri ambayo haielezi tu kwa ufasaha uwezekano mbalimbali na chaguzi za wazi kwa nchi lakini pia majaribio katika kuandaa mazingira mazuri kwa ajili ya uzalishaji wa filamu.

Hati (sera) kuhusu thamani yake inaonekana kutokosekana kwa miongozo ya lazima na visheni, kwa mfano dibaji inatambua kuwa "filamu ni njia pekee ya mawasiliano, ni njia ya elimu na burudani, jamii, habari na kuhamasisha zaidi. njia yoyote ya mawasiliano ya umma filamu inaweza kutumika kama chombo cha kuendeleza mabadiliko chanya ya kijamii kama vile kuimarisha na kujenga uhusiano mpya kati ya utamaduni na maendeleo ya taifa. "

Kwa hiyo ni dhahiri kwamba akili zinazoweka pamoja sera zinakwenda na wakati na huwa zina maono. Hata hivyo, hali ya sasa inaonekana kutoendana na hisia zinazojionesha. Hali ya utengenezaji wa filamu na matumizi inahitaji kuchukuliwa kwa tahadhari kubwa. Bila sera madhubuti hili litabaki kuwa ndoto.

Katika suala la teknolojia ya uzalishaji wa filamu nchi hii kwa sasa inarudi nyuma haraka na inaoza. Utamaduni wa kuangalia filamu za kigeni uliojengwa kwa miaka mingi unakufa na kuzaliwa kwa uangaliaji wa filamu za ndani lakini zikiwa katika maudhui ambayo bado kwa kiasi kikubwa yapo katika dhana za kigeni.

Kwa vyovyote ilivyo uangaliaji filamu /uzalishaji umeandaliwa, nchi hii haionekani kujifunga katika azimio ambalo linahitaji jitihada za pamoja za mapinduzi ya kiutamaduni yatakayothaminiwa kwa teknolojia iliyopo na ya bei nafuu.

Inaweza isiwe muhimu sana kushiriki katika mapitio ya sera ya filamu au hata miundombinu isiyokuwepo au fedha za kujikimu na utaratibu wa mitaji ya fedha za uzalishaji filamu nchini kama itafanywa kuwa mada tofauti. Kwa kweli, inahitajika semina nzima kutathmini fedha na masoko ya filamu nchini.

Pia ushiriki mchache na wa mbali kati ya Benki na soko la mitaji ni ushahidi wa kutosha wa utaratibu wa kizamani wa misaada ya fedha katika dunia ya sasa. Inatosha kusema, kiwango cha ushiriki wa misaada ya fedha katika sekta yoyote ikiwa ni pamoja na kuchukua tahadhari ya mfumo kuamua ukuaji wa uchumi, uhimili na ubora wa bidhaa unaoshindwa kuongeza uzalishaji.

Wakati huohuo, kama msingi mkuu ni dhaifu, haiwezekani kusema rasilimali watu zinapatikana kwenye tasnia ya filamu isiyo na tija. Kuna waandishi wa script, wazalishaji, mafundi wa waongozaji wengi, nchini ambao wanaweza kupambana na changamoto ya miongozo yoyote bila kujali ugumu.

Jambo moja ambalo linaonekana kwa haraka ambalo liko kati ya rasilimali watu ni tofauti na elimu ya asili. Kwa hiyo inapaswa kuangalia kuwa ubora wa elimu ya filamu inapatikana katika nchi. Je, kuna mwelekeo wa wazi na kiwango na ushawishi wa utamaduni katika mafunzo? Tuwe na sera ya filamu ambayo itahusika na mafunzo, utafiti na maendeleo kama nilivyodokeza hapo juu.

Hakuna haja tena ya kuangalia uhalali au dosari ya taasisi inayojishughulisha na filamu katika kipindi hiki cha uchumi wa kweli katika taifa letu. Tunachoweza kuzingatia ni jinsi ya kuangalia namna elimu inavyoweza kutolewa kwa walioikosa katika shule za filamu na jinsi ya kuanzisha taasisi za mafunzo ya filamu ambazo kwa sasa hazipo, jambo linaloweza kutumiwa na hali yetu ya sasa ambapo hakuna tena busara kiuchumi ili kuwekeza katika filamu. Sababu ya kuamua ni majibu mazuri ya soko kwa filamu zinazozalishwa kwa mitaji midogo.

Katika mafunzo yatakayotolewa kwenye Taasisi za filamu, mtaala lazima uzingatie pamoja na jinsi ya kupenyeza vyote, teknolojia na utamaduni ili kuzalisha kazi zenye viwango vya kimataifa katika masuala ya ubora wa mada.

Lazima isemwe kuwa filamu/video zinahitaji msingi fulani bila kujali jamii wala rangi ya asili ya kitamaduni. Kama dhana nzima ilivyo hatuwezi kuendelea kulalamika tu bila kutafakari cha kufanya, kinachoweza kujadiliwa kitakuwa na uwezekano wa kutatuliwa kwa mtazamo mpana zaidi.

No comments: