Picha zote kwa hisani ya Mwewe
NILIANDIKA wakati wa msiba
wa Kanumba kuwa umati wa watu waliojitokeza siku ya msiba wake ni ishara tosha
kuwa sekta ya filamu nchini ni kubwa na yenye nguvu kubwa lakini iliyotelekezwa
na serikali. Kama serikali itaamua kuzichukulia filamu kwa umakini mkubwa,
ikaandaa sera na kuunda chombo maalum kitakachoshughulikia filamu mfano wa kile
cha Afrika Kusini cha National Film and Video Foundation (NFVF), naamini kabisa
zinaweza kuwa chanzo kikubwa na muhimu sana katika kujenga taifa na zinaweza
kutumika kama jukwaa la kuchochea mijadala nchini kote.
Kupitia chombo chao cha
NFVF Afrika Kusini wanajivunia ‘hazina’ za sekta ya filamu ya nchi hiyo kama Tsotsi, iliyoshinda tuzo ya Academy mwaka 2006, Yesterday, filamu
nyingine iliyoshiriki tuzo za Oscar na iliyowahi kushinda katika tuzo
mbalimbali za kimataifa, na U Carmen E Khayalitsha, iliyoshinda tuzo ya Golden
Bear mwaka 2005 katika Tamasha la Filamu la Kimataifa la Berlin .
Muigizaji wa filamu ya Yesterday, Leleti Khumalo
Filamu ya Yesterday
Filamu ya Tsotsi iliyopata tuzo ya Oscar
Filamu hizi zimekuwa zikitia
chachu na hamasa kwa watengenezaji wa filamu wa Afrika Kusini kuwa wabunifu na
wenye kujali ubora. Vipi kuhusu sisi? Hivi serikali haidhani kuwa kuanzisha
chombo cha aina hii kutasaidia kutufanya tuwe na kazi nzuri ambazo siku moja
zinaweza kushinda tuzo katika matamasha makubwa na yanayoheshimika duniani?
Mbona hatujiulizi, sekta ya
filamu Tanzania inatengeneza sinema nyingi mno zinazoifanya kushika
nafasi ya tatu katika bara la Afrika, nyuma ya Nollywood (Nigeria na Ghana ), lakini ni Afrika Kusini ambayo ina mafanikio
makubwa kwenye sekta ya filamu. Kwa nini hatujiulizi kuwa sinema nyingi za
bajeti kubwa na zenye mafanikio makubwa za kimataifa zimekuwa zikitengenezewa
Afrika Kusini.
Nchi zilizoendelea kwenye sekta ya filamu duniani wanaitumia nchi hiyokama eneo muhimu la kutengenezea sinema zao, ikiwa ni
pamoja na Blood Diamond na Lord of War ambapo inaelezwa kuwa Lord of War imesaidia
sana kutangaza maeneo tajiri ya Afrika Kusini.
Nchi zilizoendelea kwenye sekta ya filamu duniani wanaitumia nchi hiyo
Tuelewe kuwa hali ya
kimafanikio ya Afrika Kusini haikuja hivihivi tu bali ilitokana na Serikali ya
nchi hiyo kutambua kuwa sekta ya filamu ni sekta yenye nguvu na inayochangia kwa
kiwango kikubwa ukuaji wa uchumi.
Kwa mujibu wa Idara ya
Biashara na Viwanda, sekta ya burudani ya Afrika Kusini ina thamani ya karibu Randi
bilioni 7.4, huku filamu na televisheni zikichangia zaidi ya Randi bilioni 5.8
katika shughuli za kiuchumi kila mwaka.
Ni wakati sasa tuamue kwa
dhati kuandaa sera ya filamu, kuwa na chombo maalum cha filamu ili filamu zetu
ziweze kututangaza vyema kimataifa, kuchangia pato katika taifa na kuvutia
utalii. Bahati mbaya bado tasnia ya filamu nchini imezongwa na matatizo
makubwa. Sekta hii inahitaji jitihada za kimtandao za ushawishi na utetezi.
Hapana shaka jitihada hizi zikiwepo zitasaidia sana kuelekeza nguvu, kasi na ari zaidi iliyopo sasa
katika jamii yetu kwenye maendeleo ya Sekta ya filamu.
Jambo linalouma zaidi ni
kuona sekta ya filamu imekuwa ni sekta ya kujikimu tu, licha ya ukuaji wa
haraka unaoonekana. Bado mavuno halisi katika kukuza pato la Taifa na hata
watayarishaji walio wengi bado hawajafanikiwa kupata matokeo mazuri kiuchumi
kupitia filamu.
Tasnia ya filamu yaTanzania inaendelea kubakia kuwa aina ndogo ya sekta ambayo
imekuwa mfano wa “kuganga njaa” ili mradi mkono uende kinywani, watayarishaji,
wasanii na watendaji wengine wanabaki wakiwa wanaitumia sekta hii kujaribu
kuweka mambo yao yaende sawa mezani, kwa maana ya kutafuta jinsi ya
kujikimu tu. Bila jitihada za dhati sekta hii kamwe haitakuwa sekta endelevu
ambayo taifa linaweza kujivunia.
Ingawa kumekuwepo juhudi nyingi kutoka kwa wadau mbalimbali kutaka sekta hii ikue na iweze kuleta tija, lakini juhudi hizo bado hazijaweza kutoa mavuno stahiki katika kile tunachoweza kuita pato linalotokana na uchumi wa kweli wa tasnia ya filamu.
Tasnia ya filamu ya
Ingawa kumekuwepo juhudi nyingi kutoka kwa wadau mbalimbali kutaka sekta hii ikue na iweze kuleta tija, lakini juhudi hizo bado hazijaweza kutoa mavuno stahiki katika kile tunachoweza kuita pato linalotokana na uchumi wa kweli wa tasnia ya filamu.
Kwa nini sekta ya filamu
iendelee kuwa sekta ya kuganga njaa? Hali hii itaisha lini? Hivi hatma ya
wasanii kuishia kulipwa pesa kiduchu (peanuts)
ambazo wala haziwasadii kujiendeleza bali zinasaidia kwa mlo wa siku chache tu
ni ipi? Filamu ni chombo muhimu sana cha kijamii na kiutamaduni kwa ajili ya kujenga
umoja miongoni mwa nchi hasa tunavyoelekea kwenye shirikisho la kisiasa la Afrika
Mashariki.
Watazamaji wa Kitanzania
kati ya wana-Afrika Mashariki wameonekana kuzipenda sana sinema zao pamoja na kuwepo kasoro nyingi na
wamekuwa na hamasa kubwa. Kama zilivyo sinema za Nigeria ambazo alama yake kubwa ya kibiashara ni Kiingereza
chao aina ya Pidgin, Kiswahili
cha kisasa cha Tanzania kinazipa utambulisho wa kitaifa filamu zetu.
Kamwe hatutakiwi kukaa tu na kusema filamu ni burudani tu, hapana. Tunapaswa kuona filamu, mbali ya kuwa ni burudani lakinikama chombo maalum kwa ajili ya maendeleo ya taifa kwa sababu ndivyo
imekuwa ikitumiwa na nchi nyingine zilizoendelea.
Kamwe hatutakiwi kukaa tu na kusema filamu ni burudani tu, hapana. Tunapaswa kuona filamu, mbali ya kuwa ni burudani lakini
Changamoto ya kukosa
ufahamu wa namna ya utengenezaji wa filamu kwa watayarishaji, wasanii wetu na
watendaji wengine, uelewa mdogo wa wasanii, ukosefu wa miundo ya soko la kuuza
kazi, tatizo kubwa la ukosefu wa mitaji ni mambo ambayo yanapaswa yabaki kuwa
historia. Haipendezi kila siku tunapolia kuhusu mambo haya haya tu, wakati tuna
mengo ya kufanya.
kwanini suala la mtaji liwe ni tatizo kubwa linaloumiza vichwa vya watayarishaji wa filamu kwa muda wote tangu Watanzania walipoanza kufanya filamu mpaka sasa? Tatizo la nchi hii ni nini hasa? Siku moja nilikuwa naongea na raia wawili wan chi jirani ambao walisema kuwa sekta ya filamu ndiyo fursa pekee ya Watanzania kujikwamua baada ya michezo mingine yote kuonekana tumeshindwa.
Kwa nini tasnia ya filamu ya
Kwa takriban miaka 10 sasa
kilio cha wasanii na watayarishaji wa filamu, mbali ya wizi wa kazi zao
kimekuwa ni ukosefu wa mtaji wa kutengeneza filamu, ingawa mwezi Septemba 1998,
ulianzishwa Mfuko wa Utamaduni na Serikali, ambao hata hivyo haukuwa na ufanisi
kwa kuwa uligubikwa na matatizo lukuki.
Madhumuni makuu ya mfuko
huo yalikuwa kuimarisha na kuiwezesha sekta ya Utamaduni (filamu zikiwemo)
kuchangia kikamilifu katika mipango ya maendeleo ya uchumi wa Taifa kwa
kuhamasisha jamii kujituma kufanya shughuli za utamaduni zenye kuchochea
ubunifu, kuzingatia ubora wa bidhaa na huduma, kuongeza kipato katika kaya na
kuhimiza ajira za kujitegemea.
Tangu mwaka 1998 ulipoanzishwa Mfuko, naweza kukiri kuwa Mawaziri wote waliopita Wizara ya Utamaduni wameshindwa kuandaa mkakati mzuri wa kusaidia upatikanaji wa pesa au kusaidia Mfuko kwa ajili ya watengeneza filamu kwa maendeleo ya Taifa, kwa sababu hakuna yeyote kati
Pia kulikuwepo madai ya
ufisadi au kutotumia pesa zilizotolewa na wahisani kwa ajili ya kuwawezesha wasanii
na wadau wa utamaduni katika kufanikisha malengo. Walionufaika aidha walikuwa
wanajuana na wahusika au ni ndugu, marafiki au maswahiba wa kibiashara. Sina
uhakika katika hilo .
Tasnia ya filamu hapa
nchini itaendelea kuwa sekta ya kuganga njaa kama hali itaachwa kama ilivyo. Ubunifu katika sekta ya burudani na sanaa -
filamu - katika nchi hii umekuwa unakwazwa na ukosefu wa fedha jambo ambalo
limekuwa ni tatizo kubwa katika jitihada za kukuza na kuendeleza sekta.
Tuanze sasa…
No comments:
Post a Comment