Sajuki wakati akiwa na afya njema
Msanii wa filamu nchini, Sadiki Juma Kilowoko (Sajuki) leo anasafirishwa kuelekea India kwa ajili ya matibabu baada ya kukamilika kwa
asilimia kubwa ya michango iliyotolewa na wasanii na wadau mbalimbali wa tasnia
ya filamu.
Msanii huyo
ataongozana na watu wengine wawili katika safari yake hiyo. Zaidi ya Shilingi milioni 25 zilikuwa zikihitajika kwa ajili ya kumtibu msanii huyo ambapo pesa iliyopatikana ni milioni 16 pamoja na tiketi tatu za ndege. Hata hivyo michango mingine inazidi kuchangishwa
na zitatumwa kwa ajili ya kuendelea na matibabu zaidi.
Akizungumza na wanahabari, Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifamba alisema mbali na
kushukuru kwa misaada iliyopatikana, alibainisha kuwa ugonjwa wa Sajuki
umewafumbua macho na kuwafanya kama shirikisho kuwa na mikakati mipya ya
kuwasaidia wasanii wanachama
wa shirikisho hilo .
Alisema kuwa kwa sasa
shirikisho hilo limeingia makubaliano na Shirika la Hifadhi ya Jamii
(NSSF) kuhakikisha kuwa wasanii wanajiunga na bima ya afya ambapo watakuwa
wakichangia Sh 20,000 kila mwezi.
Alisema kuwa katika
kuchangia fedha hizo wasanii pamoja na ndugu zao watatu watakuwa wakitibiwa
ambapo aliwasihi wasanii kujitokeza kwa wingi kujiunga na shirikisho hilo .
“Najua wasanii wengi
wanaishi maisha ya ujana na kushindwa kuangalia hatima ya uzee wao itakuwaje,”
alisema.
Alisema, shirikisho
limekubaliana na NSSF katika kuhakikisha kuwa wasanii wanaingia makubaliano ya
mikopo ya nyumba. Sajuki anasumbuliwa na
tatizo la uvimbe tumboni.
No comments:
Post a Comment