MFDI imejiingiza katika mradi wa kusisimua na wa ubunifu, ikijihusisha katika sekta mahiri ya filamu nchini Tanzania inayokua kwa kuwasaidia watayarishaji wa filamu katika kipengele ambacho kinasimamia masuala ya Elimu kupitia Burudani (Entertainment-Education).
Mchakato wa uzalishaji filamu utazingatia kujenga uwezo wa watengenezaji filamu wa ndani wa Swahiliwood, na maudhui yao ya kiElimu kupitia Burudani yatawafikia watazamaji mbalimbali kupitia mtandao mkubwa wa usambazaji wa Swahiliwood.
Mradi wa Swahiliwood ni jitihada kubwa za pamoja na wa faida kati ya Watayarishaji filamu wa Tanzania na MFDI-TZ. Ushiriki wa Watayarishaji kwenye mradi unaosimamiwa na MFDI-TZ utasaidia kupata mafanikio makubwa ya mitandao ya usambazaji wa filamu za kiElimu kupitia Burudani. Mchango MFDI-TZ kwa Watayarishaji ni kusaidia uzalishaji na mafunzo.
Mradi huo utashuhudia watengenezaji maarufu wa filamu za Kiswahili wakipitia mfululizo wa warsha, kwa njia ya mchakato wa kuzalisha filamu kwa lengo la kupeleka Elimu kupitia Burudani. Warsha itapitia mchakato wa uendelezaji wa muswada andishi (script development), maandalizi (preproduction), uzalishaji (production), uhariri (postproduction) na masoko ya filamu (marketing of films).
Mchakato wa warsha utasaidia kupeleka Elimu kupitia Burudani (ambayo wanaiita Kazi za Swahiliwood) kujiuza katika soko kutokana na ubora wa juu wa uzalishaji. Pia utahamasisha watengenezaji wa filamu kuingia kwenye miradi yao wenyewe ya Elimu kupitia Burudani.
Washiriki wa mfululizo wa warsha za Swahiliwood watakuwa Watayarishaji/Waongozaji wa Tanzania , wataowajibika na filamu kwa ujumla. Hata hivyo, hawataweza kushiriki kwa ukamilifu katika warsha zote, lakini badala yake watakuwa wanakuja kwa majadiliano katika kila hatua ya warsha.
Hivi sasa, MFDI Tanzania imekamilisha hatua mbili za warsha. Warsha ya kwanza iliwaleta pamoja wataalamu wa ndani na wa kimataifa kutoka sekta ya filamu na mashirika ya maendeleo. Watengenezaji wa filamu wa ndani kila mmoja kutengeneza muhtasari/dhana wa filamu zinazohusiana na Elimu kupitia Burudani, ambapo washiriki saba walichaguliwa ili kuendeleza hadithi zao katika miswada andishi.
No comments:
Post a Comment