Vincent Kigosi 'Ray'
Mange Kimambi
Elizabeth Michael 'Lulu'
Jinsi kifo cha muigizaji staa
wa Bongo Movies, Steven Kanumba kilivyotokea, kilikuwa lazima kiibue mshindo
mkubwa na ‘apdeti’ ni kwamba msanii mwingine wa Bongo Movie, Vincent Kigosi
maarufu kwa jina la ‘Ray’ atasimama kortini na mwanamke kiroporopo, Mange
Kimambi.
Ray, amejiapiza kuwa lazima
amfikishe Mange mahakamani kwa sababu ya kumzulia tuhuma kwamba yeye ndiye
aliyehusika na kifo cha Kanumba.
Madai ya msingi kutoka kwa
Ray ni kuwa Mange aliandika kwenye blogu yake akimtaja yeye kwamba ndiye
mhusika nambari moja wa kifo cha Kanumba. Inadaiwa kuwa Mange alichapisha maneno kuwa
aliyemuua Kanumba siyo muigizaji aliye mahabusu hivi sasa, yaani Elizabeth
Michael ‘Lulu’ ila mhusika ni Ray.
Ijumaa iliyopita, Ray
alimfungulia mashtaka Mange ya kumdhalilisha na kumchafulia jina lake kwenye Kituo cha Polisi Oysterbay. Kabla ya taarifa za
polisi, Ray alinukuliwa kwenye tovuti moja nchini akibainisha kuwa hawezi kukaa
kimya kwa sababu Mange amemchafua kwa kiasi kikubwa.
“Mimi huyo dada anayeitwa
Mange Kimambi simjui na hili suala ni zito kwa hiyo siwezi kumuacha hivi hivi,
lazima nimfikishe mahakamani,” alisema Ray, akinukuliwa na tovuti hiyo.
Akizungumza na ripota wa
gazeti moja nchini, Ray alisema kuwa mambo yote anayapeleka kisheria lakini
hakusema ni lini shauri lake litafikishwa mahakamani. Alisema: “Nilimuweka ndani leo (Ijumaa)
lakini nasikia ameachiwa kwa dhamana. Nataka mashabiki wangu wajue hata iweje
lazima nimfikishe makamani, siwezi kumuacha.
“Kanumba alikuwa mdogo
wangu, nina historia ndefu naye. Tumeshirikiana mambo mengi kuliko mtu wa
kawaida anavyoweza kukaa na kufikiri, sasa nawezaje kufanya njama ya kumuua
mdogo wangu?
“Yote kwa yote, yeye ambaye
anasema nimehusika, itabidi aithibitishie mahakama ni kwa namna gani nilihusika
na kifo cha Kanumba.”
Wakati huo leo Lulu
anatarajiwa kufikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es
Salaam kwa mara ya pili akikabiliwa na kesi ya kuhusishwa na kifo cha Kanumba.
No comments:
Post a Comment