Timu ya Bongo Movie |
Jacob Steven (JB), mwenyekiti mpya wa Bongo Movie Club
Kwa miezi kadhaa sasa tangu ile mechi ya hisani ya kwachangia waathirika wa Mabomu ya Mbagala kati ya Bongo Movie na Bongo Fleva kumekuwepo mtafaruku kati ya Bongo Movie Club na Shirikisho la filamu Tanzania (Tanzania Film Federation, TAFF), mtafaruku ambao ulitawala katika vyombo vya habari.
Kuundwa kwa Timu hii ilionekana kama ni kulipinga Shirikisho la Filamu, lakini wahusika wa Timu hii wakidai kuwa hakuna kitu kama hicho huku wakisisitiza kwamba Club hii iliundwa kwa ajili ya kufanya mazoezi kwa ajili ya Afya za Wasanii, na walio upande wa pili wakisema kuwa Bongo Movie Club ni Waasi.
Baada ya mechi ile timu hii ilirudi kwa sura tofauti kidogo kwa kuaminika kuwa ilikuwa na nyota wengi, ilianza harakati za kuandaa mechi pamoja na kushiriki katika Mabonanza mbalimbali bila kuihusisha Taff na kujizolea umaarufu mkubwa jambo lililozua mtafaruku kwenye Shirikisho ikihisi kusalitiwa.
Ndipo ikaja ile siku ya mkutano ulioandaliwa na Shirikisho katika Viwanja vya Leaders Club, tarehe 8 July 2011 ambapo wasanii wa pande zote walifika kwa ajili ya kusikiliza, na inaaminika kuwa ni siku hiyohiyo Bongo Movie Club walifanya uchaguzi wa viongozi wao na kumchagua JB kuwa mwenyekiti.
Wasanii walipokuwa makini kumsikiliza Rais wa Shirikisho hilo, Simon Mwakifwamba, aliposimama na kusema kuwa Timu ya Bongo Movie Club ni Timu ya Shirikisho na itakuwa chini ya Shirikisho. Kauli hiyo ilifurahiwa na Bongo Movie Club lakini hali ilibadilika baada Shirikisho kutoa cheti cha Usajili halali ambacho kimetolewa kwa shirikisho hilo.
Bongo Movie Club wamejitahidi kuijenga timu na kuchagua uongozi mpya lakini walisahau kuisajiri kwa kuwa hawana umiliki wowote halali wa kuweza kuwa na Timu hii, timu ina zaidi ya Miezi kadhaa bila kusajiliwa lakini baada ya Shirikisho kugundua hilo mnamo tarehe 29 June, 2011.
No comments:
Post a Comment