Baada ya Jacqueline Wolper kuzua tafrani
wasanii wengine nao waliporomosha matusi.
Rais wa TAFF, Simon Mwakifwamba akionesha
magazeti yenye habari za ngono za waigizaji,
kulia kwake ni Kulwa Kikumba (Dude)
Steve Nyerere naye akitaka kupanda jukwaani
kabla hajazuiwa na Rado
Mkutano mkubwa wa waigizaji na wadau wa filamu uliofanyika kwenye viwanja vya Leader Club Ijumaa ya tarehe 8 Julai, 2011, chini ya Shirikisho la Filamu Tanzania (Taff) ulisababisha tafrani kubwa baada ya muigizaji wa filamu, Jacqueline Wolper, ambaye pamoja na wasanii wengine nyota walihudhuria, alitoka toka sehemu aliyokuwepo na kuelekea jukwaani kwa spidi kwa ajili ya kumkwida Rais wa Shirikisho hilo, Simon Mwakifwamba (Jaspa), lakini Mabaunsa pamoja na askari walifanikiwa kumzuia ili asipande Jukwaa hilo.
Sababu ya Jack kutaka kumvamia Mwakifwamba ni baada ya Rais huyo kukemea na kutoa magazeti kadhaa ambayo yameripoti habari zinazohusiana na mambo ya ngono kwa baadhi ya wasanii hao.
(PICHA ZOTE KWA HISANI YA GLOBAL PUBLISHERS)
Katika tafrani hilo, wasanii wengine, Deogratius Shija, Steve na Simon Mwapagata (Capturado) walifanikiwa kumtoa Jack sehemu hiyo na kumpeleka pembeni kabisa ambapo Polisi walimtuliza msanii huyu.
Wakati hali hiyo ikiendelea huku kila mtu au makundi yakijadili tukio hilo la aibu kufanywa na msanii huyu kila kundi lililenga kujadili kuhusu maslahi yake, huku kundi kubwa la wasanii wa kwenye vikundi wakishangilia kwa nguvu kutokana na kauli za Rais wao na tukio hilo la aina yake. Kwa tukio la lililotokea katika viwanja hivi ni wazi kuwa hakuna amani ya kweli katika tasnia ya filamu visasi, chuki vimetawala, je sababu ni nini?
No comments:
Post a Comment