Dec 24, 2010

Sanaa na utamaduni wa Tanzania vithaminiwe

Rais Jakaya Kikwete akipiga ngoma ya kisukuma, 
moja ya tamadauni za Kitanzania 

 Kingo, moja ya majarida ya Kitanzania. 
Hapa alikuwa akitafuta Miss Tanzania wa ukweli

KADRI miaka inavyozidi kusonga mbele, ndivyo mabadiliko ya sayansi na teknolojia yanavyoongezeka nchini Tanzania, pia ndivyo jamii inavyosahau utamaduni wao kwa kuiga utamaduni wa kigeni ambao ingawa una faida, lakini matatizo ni makubwa zaidi. 
 
Tangu utandawazi ulipoanza kushamiri katika miaka ya 2000, ndivyo uigaji wa utamaduni kutoka mataifa mengine ya nje, nao uliingia kwa kasi nchini Tanzania, ambapo wananchi wengi nchini Tanzania waliacha utamaduni wao na kuiga wa nje.
 
Hali hiyo ndiyo inayoua sanaa za utamaduni nchini Tanzania ambapo wasanii mbalimbali ambao wamekulia kwenye familia hizo wanakosa soko la kuuza sanaa zao na wengine kuacha kabisa kutengeneza sanaa hizo kwa kuwa mahitaji yake ni kidogo.

Nchini wasanii mbalimbali wa sanaa za utamaduni wanalalamika ukosefu wa soko la bidhaa hizo, kutokana na wananchi wengi wa Tanzania kuonekana kupenda zaidi utamaduni wa kigeni kuliko wa kwao.  
 Ujumbe kutoka Chama cha Sanaa na Fasihi cha China 
ukiangalia vinyago mjini Dar es salaam
 

No comments: