Dec 15, 2010

BASATA yasema kuwa usajiri wa wasanii ndiyo mwanzo wa heshima katika sanaa

Sehemu ya jiji la Mwanza kilipofanyika Kikao cha nane cha Sekta ya Utamaduni

 
Mtendaji Mkuu wa Basata, Ghonche Materego
 
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Ghonche Materego amesema kwamba zoezi la usajili wa wadau wa sanaa linaloendelea nchini kote ni mwanzo wa kujenga heshima ya tasnia ya sanaa ambayo kwa miaka mingi imekuwa ikionekana kama ridhaa, isiyo na mchango wowote katika uchumi wa nchi na zaidi ya burudani tu.

Aliyasema hayo alipokuwa akizungumza kwenye Kikao cha nane cha Sekta ya Utamaduni kilichofanyika jijini Mwanza. Materego alisema kwamba, ni vema wasanii, wamiliki wa kumbi za sanaa na utamaduni na wadau wote wanaojihusisha na sekta ya sanaa
kujisajili na kuwa rasmi kwani wamekuwa kwa muda mrefu wakitengwa na watengeneza sera kutokana na mchango wao kutokuwa ukionekana moja kwa moja.

Kuhusu gharama za usajili, Materego alisema ni nafuu na zinazoweza kulipwa na wadau wote wa sanaa wakiwemo wasanii kwa kuwa vimewekwa kwa mujibu wa sheria ndogo za Basata ambazo ziliwekwa kwenye gazeti la serikali na kuthibitishwa na wizara baada ya kuonekana vinakidhi.

Kwa mujibu wa viwango vya usajili vya Basata vilivyopo, usajili unagharimu shilingi elfu thelathini huku zile za vibali zikitofautiana kulingana na wadau husika.

No comments: