Jun 30, 2011

Mafunzo ni muhimu katika tasnia ya filamu

Moja ya mafunzo ya filamu yaliyotolewa hapa nchini. 
Hapa washiriki wakibadilishana mawazo nje ya 
Kituo cha Utamaduni cha Ujerumani (Goethe Institut). 
Kulia ni mwandishi wa makala hii, Bishop Hiluka

MWISHONI mwa wiki iliyopita Tamasha la Filamu za Nchi za Majahazi (ZIFF 2010), lilihitimishwa huku kukiwa na mambo kadhaa yanayozidi kuitia doa tasnia ya filamu nchini. Katika tamasha hilo filamu zaidi ya 100 zilioneshwa sambamba na wasanii mbalimbali kutoka nchini Tanzania, Afrika na nje ya Afrika kuonesha burudani ndani ya Visiwa vya Zanzibar.

Tamasha hilo la filamu la Zanzibar lililoanza Juni 18 ndani ya Ngome Kongwe Zanzibar, likiwa linafanyika kwa mara ya 14 tokea lilipoanzishwa, limekuwa na mchango mzuri sana katika tasnia ya filamu na linapaswa kuchukuliwa kama somo muhimu sana na waigizaji, waandaaji, waongozaji na watunzi wa filamu wa Tanzania.

Jun 24, 2011

Tamasha la filamu: “Grand Malt Tanzania Open Film Festival” ndani ya Tanga kuanza Juni 27

Mkurugenzi wa Sofia Production, Mussa Kissoky (kulia)
akielezea kwenye ukumbi wa Habari MAELEZO.
Katikati ni Meneja Masoko wa TBL, Fimbo Butallah,
kushoto ni Meneja wa Grand Malt, Consolata Adam

Tamasha kubwa la wazi la filamu nchini Tanzania litakalojulikana kama 'Grand Malt Tanzania Open Film Festival' linatarajiwa kufanyika jijini Tanga kuanzia Juni 27, 2011 ambapo zaidi ya Filamu kumi kali kutoka kwa watayarishaji mahiri wa Tanzania zinatarajiwa kuoneshwa katika tamasha hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa kampuni ya
Sofia Production, Mussa Kisoki alisema tamasha hilo litafanyika katika viwanja vya Tangamano, kuanzia Juni 27 na kumalizika Julai 3 mwaka huu.

Channel mpya ya Kiswahili yazinduliwa na M-net Afrika jijini Dar es Salaam

 
Mkurugenzi Mtendaji wa M-Net Africa, Bilola Arabi
akizungumza wakati wa uzinduzi

Muigizaji maaruf wa Tanzania, Steven Kanumba 
akichanagia wakati wa uzinduzi


Juzi jioni, 22 Juni, 2011 kulifanyika uzinduzi wa channel mpya ya Kiswahili (Africa Magic Swahili) uliofanywa ndani ya hoteli ya Movenpick ya  jijini Dar es Salaam, Channel hiyo inatarajiwa kuanza kuruka hewani kuanzia Julai mosi, 2011, ambapo filamu za Bongo zitapata nafasi kubwa ya kuonekana kwenye channel hiyo.  Pia imebainika kuwa channel hiyo itakuwa ikirusha matangazo yake katika nchi zinazoongea Kiswahili ikiwemo Kenya, Uganda, Rwanda, Ethiopia, Burundi, Congo pamoja na DRC.

Waziri Nchimbi, ni kweli wasanii hawapatani, sasa?

 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, 
Emmanuel Nchimbi

Dilesh Solank, Mkurugenzi wa Steps Entertainment, 
wasambazaji wa filamu nchini wanaolalamikiwa 
kuasisi mgawanyiko wa wasanii

WIKI iliyopita, wasanii wa filamu walio chini ya mwamvuli wa Bongo Movie Club walizuru Bungeni Dodoma, walikocheza mechi ya kirafiki na timu ya wabunge, Bunge Sports Club. Ni katika hafla hiyo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi, alipokiri kuwepo matatizo ya kuelewana kwa wasanii wa filamu hapa nchini, hali ambayo inarudisha nyuma maendeleo ya sanaa.

Waziri Nchimbi aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na timu ya soka ya Bongo Movies Club baada ya kumalizika kwa mchezo wa kirafiki kati yake na timu ya Bunge Sports Club uliochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, ambapo Bunge Sports Club iliifunga Bongo Movies Club 2-1.

Jun 21, 2011

Filamu ya Maalim Seif yatikisaTamasha la filamu Zanzibar

 Maalim Seif Sharrif Hamad akiwa na Mtayarishaji Kiongozi wa Filamu yake, Javed wakati Filamu hiyo ikioneshwa katika ukumbi wa Ngome Kongwe Zanzibar

 
Maalim Seif Sharrif Hamad akiwahutubia wakazi wa Zanzibar waliofurika katika ukumbi wa Ngome Kongwe kushuhudia uzinduzi wa Filamu yake

Safari ya Makamu wa Rais wa Zanzibar kuelekea Ikulu iliyowekwa katika filamu na kampuni ya ZG na kuzinduliwa katika tamasha la 14 la Filamu visiwani Zanzibar juzi ilikuwa gumzo katika Ukumbi wa Ngome Kongwe na kuzoa umati wa watu kuishuhudia na ilizua upya hisia za kisiasa kiasi cha kumlazimu mhusika mkuu kutuliza hisia za watazamaji hao.

Filamu hiyo maalum inayoelezea maisha na harakati za maisha ya mwanasiasa huyo mkongwe ambaye ni makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad imepewa jina la A Journey to the State House na imetengenezwa na kampuni ya ZG inayojishughulisha na mambo ya filamu visiwani humo.

Pappa-Zi kufanya kongamano la filamu leo, Dar

 Rais wa TAFF, Simon Mwakifwamba

 Wasanii wa kikundi cha ABY cha Buguruni Malapa
wakiwa katika mazoezi ya sanaa

Kongamano la wadau na wasanii wa filamu Tanzania, litafanyika leo kwenye ukumbi wa Villa Park Resort jijini Dar es Salaam, pamoja na mambo mengine litazungumzia nafasi ya wasanii wa filamu nchini.

Kongamano hilo linafanyika chini ya kampuni ya Pappa-Zi ambayo ni kampuni mpya yenye madhumuni ya kuibua vipaji vya wasanii, kuendeleza na kusambaza kazi zao. Pappa-Zi imetangaza mikakati mipya ikiwa ni pamoja na kusimamia kazi za wasanii na kwa kuanzia, itakuwa jijini Dar es Salaam.

Waziri Nchimbi akiri wasanii hawaelewani

 Emmanuel Nchimbi

 Bongo Movie Club

Bunge la Tanzania mjini Dodoma

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi, amekiri kuwa bado kuna matatizo makubwa ya kutoelewana kwa wasanii hapa nchini, hali ambayo inarudisha nyuma maendeleo ya sanaa.

Waziri Nchimbi aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na timu ya soka ya Bongo Movies Club mjini Dodoma baada ya kumalizika kwa mchezo wa kirafiki kati yake na timu ya Bunge Sports Club uliochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, ambapo Bunge Sports Club iliifunga Bongo Movies Club magoli 2-1.

Nchimbi aliwataka wasanii kumaliza tofauti zao na kuwa na mshikamano na umoja ili waimarishe na kuboresha kazi zao za sanaa. Alisema (serikali) wataendelea kushirikiana na wasanii katika michezo ya kirafiki na masuala mbalimbali ya kijamii ili kujenga mahusiano mazuri kati yao (wabunge) na wasanii.