Rais wa TAFF, Simon Mwakifwamba
Wasanii wa kikundi cha ABY cha Buguruni Malapa
wakiwa katika mazoezi ya sanaa
Kongamano la wadau na wasanii wa filamu Tanzania, litafanyika leo kwenye ukumbi wa Villa Park Resort jijini Dar es Salaam, pamoja na mambo mengine litazungumzia nafasi ya wasanii wa filamu nchini.
Kongamano hilo linafanyika chini ya kampuni ya Pappa-Zi ambayo ni kampuni mpya yenye madhumuni ya kuibua vipaji vya wasanii, kuendeleza na kusambaza kazi zao. Pappa-Zi imetangaza mikakati mipya ikiwa ni pamoja na kusimamia kazi za wasanii na kwa kuanzia, itakuwa jijini Dar es Salaam.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyosambazwa juzi jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Issa Kipemba, ilisema kwamba kampuni hiyo imenuwia kufanya makubwa ikianzia kufanya kongamano hilo.
Katika kongamano hilo, Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifwamba, anatarajiwa kuwa mmoja wa watoa mada za kuhamasisha wasanii waliokata tamaa kurejea kwenye ulingo wa kufanya kazi hiyo ya kuelimisha na kuburudisha kwa malengo ya kutengeneza jamii.
No comments:
Post a Comment