Wasanii wa filamu Aunt Ezekiel na Wema Sepetu wakiwa jukwaani
INASHANGAZA sana ! Katika kipindi cha
miaka michache tu iliyopita taratibu kumeingia mdudu mbaya sana katika tasnia nzima ya burudani, huku
tasnia ya filamu ikionekana kuongoza. Tumekuwa tukishuhudia jinsi wasanii wa
kike wanavyokuwa nusu watupu kitu kinachosemwa eti ndiyo maendeleo (kupiga
hatua), na pengine inabainishwa kuwa hiyo ndiyo dalili ya kuwepo kwa mafanikio
katika tasnia hii.






