· Ni
wakati sasa mfikirie kuwa na dira
Wafanyuakazi wa Mamlaka ya Mapato (TRA) walipotembelea wauzaji wa filamu za Tanzania kuhakiki kazi zenye stempu za TRA |
Mmoja wa wasanii wa filamu Tanzania, Vicent Kigosi, maarufu kama Ray |
KWA Tanzania hakuna msanii
yeyote anayeweza kusimama na kujisifu kwamba anakula halali kulingana na wingi
wa jasho lake. Kila mmoja anatambua kuwa kuna mfumo kandamizi unaonyonya jasho
la wasanii. Na ili kuendelea kuwanyonya, sasa wameaminishwa (na wale
waliolishika soko) kuwa soko la kazi zao limekufa.
Wameaminishwa
hivyo kwa kuwa soko la kazi zao linadhibitiwa na wafanyabiashara wachache,
wasiozingatia taaluma na wasioongozwa na weledi. Ki ukweli kwa sasa soko
halieleweki kabisa! Hali hii imesababisha watu kushindwa kutofautisha iwapo
wanachokiona ni filamu, maigizo au mkanda wa harusi wenye “taito” za majina ya
wasanii na wafanyabiashara wenye asili ya Kiasia!
Kisingizio kikubwa cha soko kufa
ni kuwepo kwa filamu za nje ambazo
zinasemwa kuwa zinaharibu soko la filamu za wasanii wa ndani. Ukiachana na kisingizio hiki (ambacho binafsi sikiamini sana), hali
ya soko kwa sasa inakatisha tamaa kabisa, kiasi kwamba kuna wakati nahisi kama wasanii
(na hata viongozi wao) wengi wamefikia ukomo wa kufikiri, wameridhika au
pengine wamekata tamaa, ingawa bado wana nafasi kubwa ya kufanya vizuri zaidi!
Haiwezekani
ulilie kuthaminiwa wakati umesahau kuwa mambo yote haya ni lazima yaanze ndani
yako, kisha yaende kwenye jamii. Wasanii wengi wamekosa kujipa thamani na kujipenda, na hivyo
imekuwa vigumu kutoa kwa wengine. Wengine wengi wanahisi hawana stahili
ya mambo yote hayo. Wanajitazama wenyewe kama dhaifu kuliko wengine ama bora
kuliko wengine.
Kwa hali
ilivyo, wasanii wanapaswa wajue kwamba watu wanaoshabikia ujinga ni wachache
sana siku hizi; na watu wa maana wanaoelewa nini wanafanya ni wengi zaidi na
hawana muda na upumbavu. hivyo imefika mahali watu wanaendelea na mambo yao ya
maana, na kuupa kisogo kabisa upande wa sanaa, hasa filamu za ndani, sekta
inayoongoza kwa umbumbumbu, majungu na mambo yanayotia kichefuchefu katika
jamii.
Kielelezo cha maendeleo ya
nchi yoyote huchagizwa na ubora wa sanaa zake, hasa filamu na muziki. Wasanii
wanapokuwa na maisha mazuri na wakawa wanaishi maisha ya msanii (kuishi
kisanii), ni dalili kuwa nchi husika ina mwamko mzuri wa kiuchumi (angalia nchi
zilizopiga hatua). Utajiri wa wasanii ni utajiri wa jamii, ni utajiri wa nchi.
Wengi tunatamani sana kuona uwepo wa mazingira bora ya soko huria, ili wasanii wafanye biashara bila longolongo, watengeneze fedha, wafikie daraja la kuitwa matajiri ili tuone raha yake. Wasanii wanapofanya biashara na sanaa ikapita kwenye mkondo wake barabara, husisimua uchumi wa sekta ya Viwanda na Biashara.
Pia huitangaza nchi na kuchagiza kivutio cha wageni kutembea kibiashara au kitalii, hivyo kuipa nguvu sekta ya Utalii. Wasanii wanapotajirika, huwezesha kupanuka kwa sekta ya Uwekezaji na kutanuka kwa sekta za Ajira na Elimu.

Katika nchi yenye mfumo
bora au yenye kuwajali wasanii, wasanii huvuna stahili ya jasho lao na
kutengeneza fedha za kutosha, jambo linaloweza kupunguza msongamano wa wananchi
wanaojibana kutibu njaa katika sekta isiyo rasmi, kwani wengi wa waliopo huko,
wana vipaji sana lakini hawavitumii kikamilifu kwa kuona na kuamini kwamba
maisha kwenye sanaa ni magumu na hayalipi.
Biashara ya sanaa inaposhika nafasi stahiki na kujaa kwenye mifereji yake, inaweza kuchangamsha ubunifu kwa watu na kufanikisha kutengeneza ajira, badala ya kufikiria kuajiriwa tu. Mafanikio hasi ya wasanii wa Tanzania, ni sababu ya vipaji vingi kupotea.
Ni ukweli usiopingika kuwa kwa kiasi fulani kuna mafanikio katika sekta za filamu na muziki. Ni kweli filamu na muziki vimevuka mipaka ya Tanzania (japokuwa ni kwa nguvu binafsi za wasanii wachache). Ni kweli, filamu na muziki zinaitangaza sanaa ya Tanzania, lugha ya Kiswahili pamoja na nchi yetu. Lakini, mafanikio haya yanaweza yasionekane kwa sababu yanawabeba wasanii wachache sana, ukilinganisha na idadi ya wasanii wote nchini.
Hali
iliyopo sasa, wapo wasanii wachache mno (wa filamu na muziki) wanaopata ‘promo
mbuzi’ kwa sababu maalum. Wanapewa promo ili watumike kuuhalalisha mfumo
dhalimu uliopo, hao ndiyo huwaponda wenzao wanaolalamika kuwa hawauzi, kwamba
muziki wao au filamu zao hazikubaliki ndiyo maana wanaponda mfumo.
Pamoja na ripoti ya Shirika la Hakimiliki Duniani (WIPO) ya mwaka 2012 kuonesha mchango wa mapato uliotokana na shughuli za Hakimiliki (sanaa) kuwa zaidi ya mchango wa Sekta ya Madini, au mchango wa ajira katika kazi zilizotokana na Hakimiliki kuwa zaidi ya madini, umeme, gesi, maji, usafirishaji, mawasiliano, ujenzi, afya, na ustawi wa jamii; inasikitisha kuona bado sekta hii inaendelea kuwa duni siku hadi siku.

Naamini
kuna uchumi mkubwa sana ndani ya sanaa ila imekuwa vigumu sana kuuona au hata
kuufikia kama soko lake linakuwa limebanwa. Lazima kwanza soko liwe jepesi na
huria, wasanii watengeneze fedha na hapo ndipo itakuwa rahisi kuona manufaa
mapana ya kiuchumi ndani ya jamii na taifa kwa jumla.
Ni wakati mwafaka sasa, unapotembelea shuleni na kumuuliza mwanafunzi wa shule ya msingi au sekondari, matarajio yake nini kwa maisha yake ya baadaye, naye ajibu kuwa yeye ana kipaji, kwa hiyo anatamani kuwa msanii maarufu wa kimataifa, mwenye mafanikio na kutengeneza fedha nyingi. Msanii kwa kawaida mkondo wake ni maisha ya burudani. Starehe kwa sana!
Ni vigumu leo hii, umuulize mtoto anataka kuwa nani baadaye, naye akujibu kwamba anaota kuwa msanii mkubwa kwa sababu anapozungumza na wazazi wake, wanamwambia kazi nzuri ni Uinjinia, Udaktari, Urubani, Ubunge na ajira nyingine ambazo ni rasmi kwa sasa.
Mzazi mwenyewe anajua kwamba wasanii wanahangaika na njaa (wanaishi maisha ya kuigiza yasiyo na uhalisia). Hii ndiyo sababu mpaka leo, kila unapomuuliza swali msanii anayetambulika, alipotoka mpaka kufika alipo, atakwambia kwamba wazazi wake hawakutaka kabisa awe msanii. Si kwa sababu ni fani mbaya la hasha! Wanaona sanaa ni kupoteza muda, ni uhuni tu! Laiti wangeona mafanikio ya wasanii, wasingewakataza watoto wao hata kidogo.
Ifike wakati sanaa iwe ndiyo kimbilio la vijana wenye vipaji, na wazazi waone fahari kuwaunga mkono watoto wao pale wanapoona wanaonesha vipaji wakiwa wadogo kwa sababu ya kuamini kwamba watakuwa watu mashuhuri na wenye utajiri mkubwa.

Angalia
Marekani: Mama yake Justin Bieber, alipoona mwanaye ana kipaji cha muziki,
alimnunulia gita kwa sababu ya kuamini mwanaye anapita njia ya mafanikio. Leo
hii anafaidi matunda ya kipaji cha mtoto wake. Ifike wakati, wazazi wote wawe
na imani hiyo na wawekeze kwenye vipaji vya watoto wao.
Watu
wanashindwa kufikiria na kubuni njia ya kutengeneza fedha kupitia sanaa kwa
sababu ya kuona jinsi wasanii wanavyoishi kwa taabu. Inahitaji mtu mwenye akili
ya uthubutu kama mwendawazimu, ndiye anaweza kuona kitu fulani hakilipi na
kimewapotezea dira wengi, kisha naye akifanye kwa kuamini kitampa mafanikio.
Ni
wazi kwamba hapa Tanzania inawezekana kabisa kufikia hatua nzuri na kuona
matokeo ya faida ya sekta ya filamu, na sanaa zingine, katika ukuaji wa pato la
taifa na la wasanii wenyewe kama wasanii watafanikiwa. Kujitangaza inahitaji
fedha, msanii wa Kitanzania hawezi kujulikana kila kona ya Afrika, Ulaya, Asia,
Marekani, Australia na kwingineko kama hajitangazi. Na bila dira, malengo na mikakati
mizuri atajitangaza vipi?
Huu ni wakati sasa wasanii waandae dira itakayowaongoza kwenye mafanikio ya kisekta, ikifuatiwa na malengo yatakayofikiwa na mikakati mizuri. Katika kuboresha kazi na kujitangaza kimataifa wafikirie kuwasilisha proposals zao kwenye mamlaka za Utalii kama Tanapa, Bodi ya Utalii n.k., ili wawezeshwe, wadhaminiwe na kisha wasaidiwe kujitangaza nje ya nchi. Baada ya hapo kutakuwa na matokeo yanayoonekana.

Alamsiki.
1 comment:
naomba unijibu hili swali.
hivi tatizo kubwa liko wapi? kwenye usambazaji au utengenezaji?
Post a Comment