Oct 5, 2009

Je, unadhani wewe ni mwandishi mzuri wa skripti? SOMA HAPA...

Bishop J. Hiluka akiandaa script kwa ajili ya kutengenezwa sinema

"Like Father like Daughter..."
Magdalena Hiluka (4) pichani akijifunza kusoma. Si vibaya kuwafuatilia wanetu ili kujua vipaji walivyonavyo kwa ajili ya kuviendeleza.

Jifunze jinsi ya kuboresha uandishi wako ili kazi yako isomeke kama ambavyo msafiri asomavyo ramani.

Kila siku nimekuwa nikisisitiza kuwa sinema bora hupimwa kwa vigezo vitano; skripti nzuri, waigizaji wazuri, muongozaji mzuri, wapigapicha wazuri, na mhariri mzuri. Skripti ndiyo inayoibeba sinema, na endapo hutakuwa na skripti nzuri iliyotokana na hadithi nzuri basi ujue kuwa kazi nzima itakosa mwelekeo.



Hadithi ni ramani (kama ilivyo ramani ya nyumba) na skripti (mwongozo) ndiyo msingi wa nyumba. Kama msingi utakuwa legelege basi sidhani kama nyumba itasalimika. Ili utambulike kama mwandishi wa skripti mwenye taaluma ya uandishi (professional scriptwriter) unapaswa kuwa na sifa tisa. 

Sifa tisa zinazohitajika kwa mwandishi wa skripti:
-Analytical ability (Uwezo wa kuchambua habari): Lazima uwe na uwezo wa kugusa mahitaji halisi ya walengwa wako na uwezo wa kutofautisha mambo muhimu na yasiyo muhimu.
-Interest in diverse topics (Shauku ya kuangazia mada mbalimbali): Mwongozo mzuri (script) unahitaji utafiti wa kina na makini.
-Organizational skill (Uwezo wa kukusanya taarifa): Uwe na uwezo wa kuandaa taarifa zenye mantiki kuhusiana na kisa chako.
-Empathy for your audience (Uelewa kwa watazamaji wako): Lazima uwe umepata mafunzo ya weledi katika kuzama ndani ya mitazamo ya watazamaji wako, wanavyovipenda, mitindo yao, na maslahi yao.
-Writing skill (Ujuzi wa kuandika): Lazima uwe na uwezo wa kuandika kwa uwazi na kwa ufupi, na lazima uwe na uwezo mzuri katika sarufi.
-Ability to think visually (Uwezo wa kufikiri ): Lazima uwe na uwezo wa kuwasilisha  mawazo yako sambamba na picha, na si maneno tu.
-Creativity (Ubunifu): Ubunifu katika kufikiri unahitajika kwa ajili ya kuandika mwongozo (script) wenye mafanikio.
-Presentation and selling skills (Uwezo wa kuwasilisha na kuuza kazi): Lazima uwe na uwezo wa kuwasilisha mawazo yako kwa ufanisi kwa wateja na uwezo wa kuuza kazi yako.
-Ability to work on a team (Uwezo wa kufanya kazi kitimu): ya malengo. Kiutendaji utajikuta ukifanya kazi na watu kadhaa wenye kazi tofauti.

No comments: