 |
D. W. Griffith |
 |
Muongozaji wa filamu Tanzania, John Lister Manyara |
SINEMA za mwanzo zilijielekeza kama vile sehemu ya jukwaa
mbele ya pazia. Kamera iliwekwa katika sehemu moja na matendo yote katika tukio
zima yalifanyika ndani ya fremu moja ya kamera na kwa pigo moja (one shot). Mtazamo
wa watazamaji kipindi hicho haukutofautiana na watazamaji ambao leo wanakaa
mbele ya jukwaa wakiangalia maigizo ya jukwaani. Ni D. W. Griffith, aliyekuwa
wa kwanza kuwahamishia watazamaji katika ulingo wa sinema kwa kazi zake za “For
Love of Gold (1908)”; “The Lonely Villa (1909)”; “The Lonedale Operator
(1911)”; na iliyovutia zaidi, “Birth of a Nation (1915)”.