![]() |
Magdalena Hiluka, akiwa na miaka 4 wakati huo. Inashauriwa
kumpa hamasa mtoto katika umri mdogo ili kujenga kipaji chake
|
![]() |
Tangazo (poster) la filamu ya Mke Mchafu. |
NIANZE makala
yangu kwa kumpongeza Mtayarishaji na Muongozaji wa filamu nchini, John Lister
Manyara, kwa sinema yake “MKE MCHAFU” ambayo ni sinema pekee ya Tanzania iliyokubalika
kuoneshwa kwenye ndege za Shirika la Ndege la Emirates. Haya ni mafanikio
makubwa. Sinema hii imewashirikisha waigizaji maaruf wa Tanzania; Zuberi Mohammed
(Niva), Hisan Muya (Tino) na Blandina Chagula (Johari) na wengineo, imeongozwa
na John Lister na mimi (Bishop Hiluka) ndiye niliyeiandika. Mafanikio ya sinema
hii yananihusu kwa kiasi kikubwa.