Wasanii wa filamu wakionesha kazi bandia za filamu zinazouzwa mtaani
MWAKA uliopita 2013 kwa
tasnia ya filamu nchini tuliuaga kwa pilikapilika mbalimbali, mojawapo ikiwa ni
mkutano mkubwa wa wadau wa filamu na muziki uliofanyika 30 Disemba 2013 kwa
kuandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na Cosota, Bodi
ya Filamu, Basata, Shirikisho la Filamu (TAFF) na Shirikisho la Muziki (TMF).
Pia kulikuwepo maandalizi ya chinichini ya wasanii/watayarishaji kuandaa
maandamano makubwa ya kuishinikiza Serikali ichukuwe hatua dhidi ya maharamia
wa kazi za sanaa.
Isingekuwa busara za
uongozi wa Shirikisho la Filamu Tanzania inawezekana hivi sasa kungekuwa na tafrani,
kwani wasanii/watayarishaji hawa walikuwa kwenye shinikizo kubwa kutoka kwa
msambazaji wa filamu kuwa endapo hawatafanya hivyo, yeye atajitoa kusambaza
filamu, jambo lililowatia hofu wasanii hawa na aliwapa masharti kuwa ili
aendelee kusambaza kazi zao ni lazima wafanye maandamano yenye kulaani na
kuishinikiza serikali kabla ya tarehe 1 Januari 2014.
Iliundwa kamati ya kuratibu
zoezi zima, kuchapisha fulana na kuandaa mabango yenye jumbe mbalimbali za
kulaani, lakini walijikuta wakikwama kwa kuwa taasisi pekee inayotambulika ni
Shirikisho la Filamu Tanzania , hivyo, hawakuwa na uchaguzi ila kuufuata uongozi
wa shirikisho kwa ajili ya kuomba sapoti.
Niweke wazi tu kuwa kwa
kiasi fulani nakubaliana nao kuhusu kukithiri kwa wizi unaodumaza ubunifu na
pato la wasanii, lakini napingana nao kwenye aina ya malalamiko wanayotaka
kuyawasilisha, na niweke wazi tu kuwa binafsi sipendi kutumiwa kama ngazi na wafanyabiashara
ambao hukutumia kwa kipindi fulani, kisha wanakutupa wakishafanikiwa.
Hapa tujiulize, hivi wale
wote wanaotaka kuandamana ni kweli wanamjua mwizi wao? Kama wanamjua ni nani? Je, wanazo takwimu/ushahidi wowote unaoonesha
wanaibiwaje, wanapoteza kiasi gani kutokana na wizi huo, na serikali inakosa
pato kiasi gani kwenye wizi huo? Nijuavyo, unapotaka serikali ichukuwe hatua ni
lazima uoneshe kwenye malalamiko yako mambo hayo, hasa ukikazia kwenye suala la
kiasi gani serikali inapoteza pato, vinginevyo watakusikiliza kisha malalamiko
yako yatafungiwa kwenye makabati, na mchezo utaishia hapo.
Hivi kati ya
wasanii/watayarishaji wanaotaka kuandamana, ni nani anayemiliki kazi (filamu)?
Hakuna! Wote walishauza kazi zao kwa msambazaji. Sasa wanapotaka kuandamana eti
tunaibiwa, mwizi wetu ni nani? Yule tuliyemuuzia kazi au nani? Maana hatuna
kazi sisi! Anayepaswa kulalamika kuibiwa ni yule mmiliki wa kazi.
Sasa hapa jambo la
kushangaza na kujiuliza, kwanini mmiliki wa kazi hataki kujitokeza kulalamika
au kuandamana na badala yake anajificha kwenye mgongo wa wasanii kwa kututaka
sisi tuandamane na kulalamika kwa niaba yake? Kuna nini hapa kinaendelea?
Nawashauri wasanii kabla hatujataka kuandamana ni bora tukarejea kwenye
mikataba yetu na msambazaji ili tujiridhishe kama ni sisi ndiyo tunaoibiwa, na tunaibiwaje ili tusije tukaingizwa
mkenge.
Vinginevyo tungeandamana na
kulalamika kuhusu mikataba hii ya kinyonyaji inayotufanya kudhulumiwa haki
zetu, lakini si kwa sababu ya wizi wa kazi zisizokuwa zetu ambao wala hatuna
takwimu zozote kuhusu kiasi cha kazi kinachouzwa, pato la shilingi ngapi
linaingia, au kiasi gani kinapotea kutokana na wizi huo.
Ninatambua wazi kuwa katika
biashara yoyote ile siku zote, katika makubaliano ya kazi, ni muhimu sana pande zote kuwa na haki na wajibu wa kila upande
katika mkataba wa makubaliano wanaoingia baina ya pande mbili. Katika jambo
hili, umakini wa hali ya juu huwa unahitajika sana ili kuepusha upande mmoja kuumizwa.
Inafahamika wazi kwamba
katika suala la mikataba ni vyema kushirikisha wanasheria ambao ndiyo wataalam
wa mikataba ili kuepuka kudhulumiwa, lakini pia kutokana na viwango vya elimu
vya wasanii wengi katika nchi hii, ni muhimu kuwa na wasimamizi (mameneja)
wanaoelewa masuala ya mikataba.
Ni vyema wasanii wakatambua kuwa kilio wanacholia cha kuibiwa si kweli, wengi wanaingia kwenye mkumbo wa wachache wanaotumiwa na wasambazaji (ambao walishawauzia haki zote) ili ionekane kuwa biashara ya filamu si nzuri na kuleta punguzo la kodi kwa wasambazaji hawa. Na hata
Aliyekuwa Katibu Mtendaji
wa Baraza la Sanaa la Taifa, Ghonche Materego, aliwahi kusema kwamba ni vyema
vyama vya sanaa na mashirikisho kuwa na wanasheria ambao watasimamia shughuli
za wasanii wao, ikiwemo kuwaongoza katika kuingia mikataba. Ghonche aliamini
kuwa kwa kufanya hivi, wasanii wataweza kujiamini katika utendaji wa kazi zao, kwani
hawatakuwa na wasiwasi wa kunyanyasika pindi washirika wao katika mikataba
watakapoonekana wanakengeusha mambo.
Nakubaliana kabisa na Mzee Ghonche lakini sijui
Wasanii wengi wamejikuta
wakidhulumiwa au kupata malipo madogo kutokana kuendekeza njaa na kuwa na
uelewa mdogo katika kuingia mikataba na baadhi ya watayarishaji/wasambazaji wa
filamu hapa nchini. Suala la mikataba limekuwa likipuuzwa sana na Watanzania wengi (si wasanii tu), hasa
linapokuja suala la kusoma vipengele na kuelewa vinamaanisha nini. Wengi
hukimbilia kuangalia sehemu inayotaja pesa tu na wakiona pesa nyingi basi husaini
bila hata kujali maeneo mengine muhimu.
Hali hii imemkumba jamaa yangu siku za hivi karibuni ambaye aliamua kuja kuniona ili kupata usaidizi baada ya kulizwa na kampuni moja kubwa ya usambazaji wa filamu. Amejikuta akiingia mkataba mbovu ambao sijawahi kuushuhudia katika maisha yangu. Mkataba wake alionionesha ambao ni wakusambaza kazi yake moja, kwa kuuangalia tu niligundua kuwa ulikuwa umetengenezwa na mwanasheria wa msambazaji huyo kwa jinsi ulivyokuwa umepangiliwa kitaalam lakini katika namna ya ujanja ujanja, tena kwa lugha ya Kiingereza. Kibaya zaidi alipopewa alitakiwa kuusaini palepale na wala hakuruhusiwa kutoka hata nao nje kabla hajausaini, ingawa alipewa nakala ya mkataba huo baada ya kusaini. Hili limekuwa ni tatizo ambalo wasanii wote wanatakiwa kulitatua wenyewe, na wala si suala la kuilalamikia serikali.

Mikataba ya aina hii
imesababisha vilio, malalamiko na kesi za ajabu ambazo kimsingi zingeweza
kuepukika endapo kungekuwa na umakini kabla ya kuingia mkataba husika.
Bahati mbaya wasanii wetu
wamekuwa hawajifunzi kabisa kutokana na makosa ya wengine, kwani inapotokea
mwenzao kaingia mkataba wa aina hii utashangaa hata watu wake wa karibu nao
hurudia makosa kama hayo, kiasi kwamba suala hili limekuwa kama ni desturi kwa wasanii wetu.
Inakuwa vigumu kuelewa kama wanafanya shughuli zao kwa mazoea na si kitaalam, kwa maana ya kuifanya kazi yao kama ajira yao rasmi ambayo inawaingizia kipato kwa kujikimu na kuendesha maisha yao ya kila siku. Kukubali mikataba isiyo na maslahi kwao imekuwa ni sawa na kujimaliza wenyewe.

Kuhusu maisha duni na
kudhulumiwa kwa haki zao, kunasababishwa na ubinafsi, kutokuwa na umoja katika
kushinikiza haki zao, kutumia vibaya kile wanachokipata kwa anasa na kutotaka
kujifunza juu ya haki zao mbalimbali kutokana na kulewa umaarufu na kukimbilia
mafanikio ya haraka haraka.
Wasanii wachache wenye maendeleo ni wale wenye kupenda kuingia mikataba ambayo ama wameipitia kwa umakini au wamepata ushauri wa kisheria kutoka kwa wataalam wa sheria, na huingia mkataba hiyo kwa kila kazi wanazofanya na huwa na nakala za mikataba hiyo. Na ni vizuri zaidi mkataba huu ukawa umepitia mikononi mwa watu wanaoweza kuutafsiri.

Jambo jingine la ajabu ni
pale wasanii wengi wanapodai kuwa na mikataba lakini wao wenyewe huwa hawana
nakala za mikataba hiyo, na hasa mikataba inayohusu usambazaji wa kazi zao,
kuna aina ya ujanja ujanja ambao hufanyika ambapo wasanii wengi huambiwa waache
mkataba kwa wasambazaji ili ukasainiwe na mwanasheria na baada ya hapo wengi
huwa hawauoni tena mkataba wao.
Tafakari…
No comments:
Post a Comment