![]() |
Watu wakiangalia sinema |
LEO nimekumbuka mbali
sana, hasa baada ya kupita sehemu na kuwasikia wanafunzi wa shule ya msingi
(wenye miaka isiyozidi kumi), ambao wapenzi wa sinema, wakisimuliana na
kubishana kuhusu kina Ray, Kanumba, Gabo nk. Ndipo nikakumbuka nilipokuwa
katika umri huo tulikuwa pia tukisimuliana na kubishana kuhusu kina Amitabh Bachchan, Mithun Chakrabot, Amjad
Khan, Dharmendra, Sanjeev Kumar, Charlie Chaplin, nk.
Wakati huo hatukuwa na
vituo vya televisheni kama leo. Vituo vya televisheni Tanzania Bara televisheni
vimeanza mwanzoni mwa miaka ya 1990. Hadi 1996 kulikuwa na vituo vitatu tu vya
CTN, DTV na ITV. Hata hivyo, televisheni imekuwapo Zanzibar tangu mwaka 1973.