![]() |
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye |
WIKI iliyopita kwenye gazeti la Raia Mwema kulikuwa na
makala yenye kichwa: “Baraza jipya la
mawaziri, mkorogo usio hamasa kwa mabadiliko”, kutoka kwa mwandishi
ninayemheshimu, Joseph Mihangwa. Nimekuwa msomaji mkubwa wa Mzee Mihangwa
(kwangu ni sawa na baba’angu), kwa miaka mingi, nimekuwa msomaji wake na
sijawahi kufikiria kumkosoa. Lakini nadhani ameteleza kidogo kwa kubeza juhudi
za wasanii wa nchi hii.