![]() |
Wasanii waliopo katika kampeni ya Mama Ongea na Mwanao mpigie kura Dk. Magufuli |
KAMPENI za Uchaguzi Mkuu wa mwaka
huu zimepambwa zaidi na wasanii mbalimbali. Kumekuwepo na mhemuko wa ajabu wa
wasanii kujitokeza kwenye majukwaa ya siasa, wengi wao wakijipambanua kuwa
wafuasi au mashabiki wa vyama na wanasiasa fulani. Zikiwa zimesalia siku 22 tu kabla
ya kupiga kura kuichagua serikali ijayo (Rais, Wabunge na Madiwani), hali bado
ni ya mashaka kwa sekta ya sanaa.
Wasanii wanatumika kwa kiasi
kikubwa kwenye majukwaa ya siasa, kiasi cha mikutano kugeuka kuwa matamasha ya
burudani, huku wakiwa hawajui majaliwa yao kuhusu ustawi wa sekta ya sanaa,
zaidi ya kupigwa porojo na ahadi zisizotekelezeka.