![]() |
Bishop Hiluka, Simon Mwakifwamba na Michael Sangu
wakati wa harakati za kupigania ukombozi wa msanii
|
HISTORIA
huwa haina haja na wale wote wenye kushindwa, labda tu kunukuu tarehe
walizokutwa na umauti wao... Sekta ya filamu Tanzania ambayo ilionekana kupiga
hatua siku hadi siku, siku za karibuni imeonekana kuanza kudorora. Ipo chumba
cha wagonjwa mahututi (ICU).
Ni ukweli usiopingika,
sekta ya filamu ipo chumba cha wagonjwa mahututi ikisubiri kupelekwa mochwari,
hasa kama hatua za makusudi hazitachukuliwa kunusuru hali hii, hali ambayo
kwangu ni kama mazingaombwe.