![]() |
Simon Mwakifwamba, Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania |
Dilesh Solanki, Mkurugenzi wa Kampuni ya Steps Entertainment |
HALI ya tasnia ya filamu nchini kwa sasa inakatisha
tamaa, wasanii na viongozi wao wengi wamefikia ukomo wa kufikiri, wanaonekana kuridhika
na hali ilivyo au pengine wamekata tamaa, ingawa bado wana nafasi kubwa ya
kufanya vizuri zaidi. Vyombo vya kuwasimamia, likiwemo Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF),
vimekosa dira.
Ni wasanii wenyewe kupitia
chombo chao, ndiyo wamesababisha sekta hii ishuke kutokana na tabia zao, hii
inawagusa wasanii wote, wanawake na wanaume. Wamechukulia kada hii kama sehemu
ya kujitangaza zaidi kuliko kazi, viongozi wao wanachukulia nafasi zao kama
fursa ya kuwakutanisha na wakubwa au matajiri ili wapige vibomu, ilimradi siku
ziende.