Paulynus R. Mtendah, mjumbe mteule wa Bunge la Katiba akiwakilisha wadau wa sanaa na filamu
BUNGE la katiba litaanza
vikao vyake Jumanne ya wiki ijayo kwa mujibu wa taarifa rasmi. Vikao vitaanza
baada ya Rais Jakaya Kikwete kufanya uteuzi wa wajumbe 201 wa bunge hilo hivi karibuni, ambapo tasnia ya filamu na sanaa kwa
ujumla imefanikiwa kupata wawakilishi watatu: Maria Sarungi, Asha Mtwangi na
Paulynus Mtendah.
Maria Sarungi ni mdau na
mtayarishaji wa filamu na masuala ya burudani kwa ujumla, Asha Mtwangi ni mdau
muhimu wa tasnia ya filamu na katibu wa Bodi ya TAFF Trust Fund, iliyo chini ya
Shirikisho la Filamu Tanzania, na Paulynus Mtendah ni mtayarishaji wa filamu na
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Waongozaji wa Filamu Tanzania.
Ni wazi kuwa Bunge la Katiba
hii litatekwa na wanasiasa na katiba itapitishwa kwa maslahi na utashi wa
kisiasa zaidi huku ikipuuza mambo mengine ya msingi kwa jamii, hasa wasanii.
Ukiisoma Rasimu ya Katiba tangu mwanzo hadi mwisho utagundua kwamba utamaduni
hauna nafasi kabisa katika nchi hii kwa sasa licha ya kuambiwa kuwa ndiyo roho
ya Taifa. Ni wakati sasa tunapaswa tuwe na na Wizara ya Utamaduni wa Taifa na Vijana
kama kweli tunataka utamaduni uwe roho ya Taifa.
Kutokana na nafasi hii
tuliyopata, wawakilishi wetu waitumie fursa hii kupigania masuala ya sanaa na
utamaduni kwa kuwa hakuna mwanasiasa yeyote atakayeongelea masula ya sanaa wala
utamaduni, kila mmoja anafikiria siasa tu. Kila kona unakopita utasikia
majadiliano juu ya muundo wa muungano, tume ya uchaguzi na mengineyo.
Kwa kudharau utamaduni
tunasahau kuwa sanaa ni zao la matokeo ya juhudi za wasanii katika kutoa
ujumbe, kukidhi matumizi na mahitaji ya binadamu, na hii kama tanzu muhimu ya utamaduni wala si kitu kilichoibuka tu. Sanaa ndicho
chombo ambacho jamii zisizokuwa na jadi ya kusoma na kuandika inatumia katika
kuhifadhi na kuwasilisha kumbukumbu za mambo muhimu katika maisha yao .
Tutambue kuwa sanaa ni kazi ya ubunifu tena yenye ufundi na mvuto kama sumaku, kazi nzuri ya sanaa ni ile iliyo na ubunifu, uasili na inayotumia mbinu bora ya uwasilishwaji wa ujumbe kwa hadhira.
Sanaa zetu za ufundi wa asili zimesahaulika na tumepokea zile za nje na hali hii imesababisha watanzania kuwa watazamaji wa vituo vya sanaa za nje badala ya kuweka nguvu zaidi katika kubadili fikra zetu ili bidhaa zetu za ufundi ziendane na matakwa ya dunia kwa kuziboresha sanaa zetu za asili. Jambo la msingi ni kuhakikisha tunazingatia, tunazitambua na tunazilinda sanaa zetu ili zisipoteze uasili wake pamoja na wimbi la mabadiliko ya wakati na mazingira ya sasa ya utandawazi na biashara huria.
Sanaa kama nguzo mojawapo muhimu ya Utamaduni hukua na pia hufa. Kwa kuudharau
utamaduni, sanaa zetu kwa sasa zinakufa au pengine zipo katika chumba cha
wagonjwa mahututi, tusipochukua juhudi za ziada tutazika kabisa uasili wa sanaa
zetu tulizopokezwa na wazee wetu kutoka kizazi hadi kizazi?.
Kwa kuupuuza utamaduni wetu,
sanaa zetu zilivyo leo haziweki kumbukumbu nzuri itakayorithiwa na vizazi
vijavyo, na kama kuna kumbukumbu basi ni kumbukumbu potofu. Kwa
kudharau utamaduni kumesababisha leo hii tumekuwa tukisikiliza nyimbo za
matusi, filamu na nyimbo za mapenzi au zisizo na asili yetu bali zilizonakili
vitendo na maudhui ya jamii za nje.
Idara ya Utamaduni ina dhina
ya kuongoza, kusimamia, na kudhibiti shughuli za ukuzaji wa Sanaa za Filamu, Maonyesho,
Ufundi na Muziki; kusimamia ukuzaji wa lugha ya Kiswahili, lugha za Asili na za
Kigeni; na kusimamia shughuli za Mila na Desturi. Tuache kulalamika na tuchukue
hatua sasa kuunusuru utamaduni na sanaa zetu.
Ukiangalia kwa kina kuhusu
utamaduni wa nchii, utagundua kupuuzwa kwake, japo baada ya uhuru mwaka 1961,
iliundwa Wizara ya Utamaduni wa Taifa na Vijana, mwaka 1962, Rais wa kwanza wa
Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere alitamka wazi kuwa Utamaduni ni kiini na roho
ya Taifa, nchi inayokosa utamaduni wake ni sawa na mkusanyiko wa watu usiokuwa
na roho na hivyo kukosa sifa ya kuitwa taifa kamili.
Sera ya utamaduni
ilizinduliwa Agosti 23 mwaka 1997 mjini Dodoma ikiwa ni hatua ya pili muhimu baada ya ile ya kuundwa
kwa Wizara ya Utamaduni wa Taifa na Vijana mwaka 1962.
Cha kushangaza, pamoja na umuhimu uliopo katika suala la utamaduni kwa maisha ya watu bado sera ya utamaduni imepewa nafasi finyu mno katika serikali yetu tangu ilipoanzishwa wizara ya kushughulikia masuala ya sanaa. Na hata rasimu ya Katiba mpya imeonesha kutokuupa nafasi kabisa utamaduni.
Cha kushangaza, pamoja na umuhimu uliopo katika suala la utamaduni kwa maisha ya watu bado sera ya utamaduni imepewa nafasi finyu mno katika serikali yetu tangu ilipoanzishwa wizara ya kushughulikia masuala ya sanaa. Na hata rasimu ya Katiba mpya imeonesha kutokuupa nafasi kabisa utamaduni.
Pamoja na kuwepo kwa sera
ya utamaduni (ingawa nayo ina mapungufu mengi), inabidi wadau wote wa sekta ya
utamaduni wajiulize, je umma wa Watanzania umefikishiwa machapisho ya sera hii
ya utamaduni ili waisome na kuielewa?
Je umma umeelimishwa kikamilifu juu ya sera hii ili uweze kushiriki katika utekelezaji kwa upana wake? Na je ushirikishwaji wa vyombo vya habari katika kusaidia msukumo wa wananchi kuielewa sera ya utamaduni umepewa nafasi ya kutosha?
Mipango ya Maendeleo imekuwa ikibuniwa na kutekelezwa bila kujali utamaduni wa wananchi, utamaduni haupewi dhima katika uamuzi na mipango ya maendeleo kwa sababu inaaminika kuwa maendeleo ni kuondokana na mambo ya kiasili pasipo kuchunguza misingi ya mambo hayo na faida zake.
Je umma umeelimishwa kikamilifu juu ya sera hii ili uweze kushiriki katika utekelezaji kwa upana wake? Na je ushirikishwaji wa vyombo vya habari katika kusaidia msukumo wa wananchi kuielewa sera ya utamaduni umepewa nafasi ya kutosha?
Mipango ya Maendeleo imekuwa ikibuniwa na kutekelezwa bila kujali utamaduni wa wananchi, utamaduni haupewi dhima katika uamuzi na mipango ya maendeleo kwa sababu inaaminika kuwa maendeleo ni kuondokana na mambo ya kiasili pasipo kuchunguza misingi ya mambo hayo na faida zake.
Kwa kiasi fulani uhusiano
kati ya utamaduni na maendeleo ulitambuliwa na Serikali ya Tanzania katika miaka ya 70. Kwa mfano, iliyokuwa Wizara ya
Utamaduni wa Taifa na Vijana (1979) iliwateua wataalam wake kadhaa waandike
kitabu kiitwacho Utamaduni Chombo cha Maendeleo. Katika dibaji ya kitabu hicho,
aliyekuwa Waziri wa Wizara husika alitoa maelezo yanayojaribu kuonesha uhusiano
kati ya utamaduni, uhuru na maendeleo. Nanukuu:
“Kuna sababu nyingi za
kuutambua Utamaduni kuwa ni chombo ni maendeleo. Moja ni kuwa vipengele na fani
mbalimbali za Utamaduni ndizo zilizoko katika kiini cha Umoja wa jamii.
Utamaduni ni sehemu ya siasa ya Taifa letu lenye msingi na shabaha ya Umoja wa
kweli. Uhuru wetu uliletwa na Umoja. Maendeleo hayapatikani bila ya uhuru na
Umoja. Hivyo Utamaduni kama Nguzo ya Umoja, ni chombo cha maendeleo (Wizara ya
Utamaduni wa Taifa na Vijana, 1979, uk. vii)”.
Miaka minane baadaye Serikali ilianzisha Baraza la Sanaa la Taifa na Baraza la Muziki la Taifa, ambayo yaliunganishwa mwaka 1984 kuwa Baraza la Sanaa la Taifa la sasa (Basata). Madhumuni ya Basata na mabaraza yaliyolitangulia, ni kufufua, kuendeleza na kukuza sanaa za asili za Watanzania.
Aidha, Chuo Kikuu cha
Chuo cha Sanaa Bagamoyo,
sasa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSUBa), kilianzishwa mwaka 1981 kwa lengo
la kutoa mafunzo kwa wasanii. Aidha mwaka 1985 serikali ilianzisha matamasha na
mashindano ya fani mbalimbali za utamaduni kuanzia ngazi ya wilaya, mkoa, kanda
hadi taifa.
Tuelewe kuwa Utamaduni huipa jamii utambulisho. Sura na haiba ya jamii huweza kueleweka na kuelezeka kutokana na utamaduni wa watu wake. Utamaduni hurithishwa kutoka kizazi hadi kizazi kupitia lugha, sanaa na imani za kiroho. Mila na desturi wanazofuata, matamasha au sherehe wanazoendesha, mavazi
Utamaduni ndiyo “kidhibiti mwendo” kinachoongoza mwenendo na tabia za watu katika jamii. Ndiyo msingi wa maisha ya mtu binafsi. Humuwezesha kujitambua, kuwa na mwelekeo na kujichagulia falsafa sahihi ya maisha yake. Ndiyo msingi wa maendeleo na ubunifu katika jamii. Maendeleo ya uchumi katika maana yake pana ni matokeo na sehemu ya utamaduni wa watu. Maendeleo yasiyojengwa katika misingi ya utamaduni wa jamii ni maendeleo yasiyokuwa na maana kwa jamii hiyo.
Alamsiki.
No comments:
Post a Comment