Nov 30, 2010

Jukwaa la Sanaa Basata: Michuzi ahamasisha wasanii kujiunga na mtandao jamii

Muhidin Issa Michuzi akionesha namna mtandao wa youtube unavyofanya kazi

MUHIDINI Issa Michuzi, ambaye ni mwandishi wa habari mwandamizi nchini amewashauri wadau wa sanaa hasa wasanii kuingia kwenye matumizi ya teknolojia ya mtandao jamii ili kujitangaza na kuuza kazi za sanaa duniani kote.

Akizungumza kwenye Jukwaa la Sanaa jana, jukwaa ambalo hufanyika kila Jumatatu kwenye ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Ilala Shariff Shamba jijini Dar,

Michuzi aliweka wazi kwamba blogs zimekuwa zikitembelewa na watu mbalimbali duniani na kuwataka wasanii kuzitumia kwa ajili ya kujitangaza, kusambaza kazi zao na hata kujitambulisha katika masoko ya kimataifa.

Alisema kuwa, blogs tofauti na aina nyingine mitandao jamii inatumiwa kuhifadhi picha nyingi na kazi mbalimbali, kupata taarifa kuhusu tasnia ya sanaa, kupokea mawazo ya wateja wa kazi za sanaa na hata kuwa na wasaa wa kuwasiliana na wasanii wengine na hivyo kupanuka kimawazo na kiujuzi.

 

1 comment:

Anonymous said...

Ni kweli, wasanii wanatakiwa kujitangaza kimataifa kwa njia ya mtandao kama kweli wanataka kwenda na wakati vinginevyo wataendelea kusota.