Rais mteule, Simon Mwakifwamba
Makamu wa Rais, Suleiman Ling'ande
Viongozi wapya na wajumbe wa Bodi ya TAFF katika
picha ya pamoja, muda mfupi baada ya kuchaguliwa
Baada ya kuwepo kwa uongozi wa mpito, hatimaye siku ya Alhamisi Desemba 22, 2011, Shirikisho lilipata viongozi wapya kwa njia ya kidemokrasia watakaoongoza kwa kipindi cha miaka mitatu hadi 2014.
Simon Mwakifwamba aliyekuwa rais wa mpito ndiye aliyechaguliwa kuwa Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania baada ya kupita kwa kishindo kwa kupata kura zote 18 za wajumbe waliopiga kura baada ya kuwa mgombea pekee mwenye sifa za kugombea nafasi hiyo kwa mujibu wa katiba ya shirikisho.
Nafasi ya Makamu wa Rais imechukuliwa na Suleiman Ling’ande baada ya kupata kura 15 na kumwangusha mpinzani wake, Daniel Basila, ambaye aliambulia kura mbili tu, huku kura moja ikiharibika.
Wajumbe wa Bodi ya Shirikisho waliochaguliwa ni Wilson Makubi, Michael Sangu, Christian Kauzeni, Makame Bajomba, Emmanuel Myamba, John Kallage, Ali Baucha, Mwanahamisi Hela, Deo Songa na Maurine Mvuoni.
No comments:
Post a Comment