![]() |
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fissoo, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Waandishi wa Filamu kwa baadhi ya waandishi hao Jijini Dar es Salaam hivi karibuni. |
MWANDISHI mzuri wa filamu ni lazima awe na kipaji na uwezo
mzuri wa kuandika. Kipaji mtu huzaliwa nacho au hukipata (adapt) katika umri
mdogo kutokana na mazingira anayokulia. Uandishi mzuri wa filamu huanzia katika
kuwa na uwezo wa kuumba maneno ambayo yatakuwa rahisi kueleweka pindi mtu
akiyasikia.
Wakati unaandika ni muhimu sana kuzama ndani ya akili za
walengwa wako ujue wanataka nini.