![]() |
Mwandishi wa makala haya, Bishop Hiluka, katika moja ya kazi za uandishi wa filamu |
FILAMU
ni chombo muhimu sana cha mawasiliano katika jamii na ustawi wa nchi yoyote,
huchangia kupatikana kwa ajira kwa vijana, huchangia ukuaji wa uchumi wa nchi,
husaidia kuwaambia watu wengine kuhusu hadithi za jamii husika, huchangia maendeleo
ya nchi na kadhalika.
Utengenezaji
wa filamu si suala la mzaha, si jambo la mtu ambaye jana usiku alilala akiwa
hana kazi ya kufanya na leo asubuhi kaamka akiwa na wazo la kutengeneza filamu,
bila kuwa na ujuzi, nyenzo wala mtaji wa kutosha. Utengenezaji filamu ni jambo
linalohitaji gharama, ni jambo la hatari (venture) linalohitaji muda mwingi na
mtengenezaji wa filamu hatakiwi kuwa mvivu wa kufikiri au kupoteza muda akipiga
soga na rafiki zake au kufanya mizaha.